DaxibotulinumtoxinA

DaxibotulinumtoxinA, inayouzwa kwa jina la chapa Daxxify, ni dawa inayotumika kuboresha mwonekano wa mikunjo inayopatikana kati ya nyusi. [1] Inaweza pia kutolewa kwa ajili ya kutibu ugonjwa sugu wa neva unaosababisha shingo kugeukia kushoto, kulia, juu, na/au chini bila hiari (cervical dystonia).[2] Dawa hii inatolewa kwa njia ya kudunga sindano kwenye misuli.[1] Madhara yake yanaweza kudumu kwa hadi miezi sita.[2]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na maumivu ya kichwa, kuanguka kwa kope na shida ya kusonga uso.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha matatizo ya kumeza au kupumua.[1] Ni sumu ya botulinamu A (botulinum toxin A) ambayo huzuia kutolewa kwa asetilikolini (acetylcholine) na ni ajenti ya kuzuia neva za fahamu (neuromuscular blocking agent).[1]

DaxibotulinumtoxinA iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2022.[1] Ni mshindani wa kibiashara kwa Botox.[3]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 "Daxxify- botulinum toxin type a injection, powder, lyophilized, for solution". DailyMed. 19 Septemba 2022. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Septemba 2022. Iliwekwa mnamo 27 Septemba 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 Solish, N; Carruthers, J; Kaufman, J; Rubio, RG; Gross, TM; Gallagher, CJ (Desemba 2021). "Overview of DaxibotulinumtoxinA for Injection: A Novel Formulation of Botulinum Toxin Type A.". Drugs. 81 (18): 2091–2101. doi:10.1007/s40265-021-01631-w. PMID 34787840.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "U.S. FDA declines to approve Revance's frown-line treatment". Reuters (kwa Kiingereza). 15 Oktoba 2021. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 17 Januari 2022. Iliwekwa mnamo 13 Desemba 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu DaxibotulinumtoxinA kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.