Dekha Abdi

Mwanaharakati wa amani wa Kenya

Dekha Ibrahim Abdi ni mfanyakazi wa huduma za jamii na amani nchini Kenya aliyepokea Tuzo Mbadala ya Nobel (Right Livelyhood Award) ya 2007.

Dekha Abdi ni mwenyeji wa Wajir katika Kenya ya Kaskazini alikozaliwa mw. 1964. Tangu 1992 alijishughulisha na matatizo ya kurudisha amani katika mapigano kati ya vikundi vya eneo la Wajir akaanzisha Kamati ya Amani ya Wajir (Wajir Peace Comittee).

Tangu shuleni Dekha ambaye ni Mwislamu alijenga uhusiano mwema na Wakristo. Uhusiano huo aliimarisha wakati wa fitina za Wajir za mwaka 1998 wakristo mjini waliposhambuliwa na vijana Waislamu. Dekha alishiriki katika kuanzisha kamati ya usaidizi iliyounganisha wakina mama Wakristo na Waislamu waliokutana pamoja kwa sala na majadiliano. Kutoka hapa kamati ya kimadhehebu ya dini zote ikaundwa liliyosaidia kukomesha hasira kati ya waumini wa dini mbalimbali.

Tangu 1996 Dekha amefanya kazi kabisa katika miradi mbalimbali za kujenga amani na maelewano akiweka uzito upande wa ushirikiano kati ya dini na imani katika Kenya ya Kaskazini, kitaifa, kibara na kimataifa.

Juhudi zake zikaheshimiwa sasa kwa kutolewa tuzo ya Right Livelyhood Award inayojullikana zaidi kama Tuzo Mbadala ya Nobel.

Viungo vya Nje

hariri