Difluprednate
Difluprednate (DFBA), inayouzwa kwa jina la chapa Durezol ni kotikosteroidi inayotumika kutibu maumivu na mwasho kufuatia upasuaji wa macho.[1] Inatumika kama tone la jicho.[1] Wale wanaoitumia hawapaswi kuvaa lensi za mawasiliano.[1]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na mwasho wa kope, hisia kali dhidi ya mwanga na uwekundu wa macho.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha shinikizo la macho kuongezeka, hali ya macho ambapo lensi ya jicho inakuwa mbaya na kupunguza uwazi wake (cataracts), uponyaji wa polepole na maambukizi.[2] Usalama wa matumizi yake katika ujauzito hauko wazi.[2]
Difluprednate iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2008 [1] na inapatikana kama dawa ya kawaida.[3] Nchini Marekani, mililita tano inagharimu takriban dola 60 kufikia mwaka wa 2021.[3] Hapo awali, ilitengenezwa kutoka kwa prednisolone.[1]
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 "Difluprednate Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 29 Septemba 2021. Iliwekwa mnamo 24 Desemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 2.0 2.1 "DailyMed - DIFLUPREDNATE- difluprednate ophthalmic emulsion". dailymed.nlm.nih.gov. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 11 Januari 2022. Iliwekwa mnamo 26 Desemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 3.0 3.1 "Difluprednate Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 19 Mei 2016. Iliwekwa mnamo 26 Desemba 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Difluprednate kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |