Kiendeshi diski kuu

(Elekezwa kutoka Diski kuu)

Diski kuu au kiendeshi diski kuu ni sehemu ya kompyuta ambako kumbukumbu ya habari hutunzwa. Inaitwa pia kwa kifupi chake cha Kiingereza HDD (hard disk drive) au HD (hard drive). Inaitwa diski kuu kwa sababu komputa hutumia diski mbalimbali kwa mfano CD au diski ndogo aina ya flopi.

Sanduku la diski kuu iliyofunguliwa; diski yenyewe na mkono wa kuandika-kusoma vinaonekana
Sanduku la diski kuu(3.5")

Muundo wa HDD

hariri

Diski kuu kwa kawaida inaonekana kama sanduku ndogo ya metali iliyofungwa kabisa. Ndani yake kuna diski inatunza kumbukumbu ya habari yote yaliyowekwa mle. Sanduku imefungwa kabisa ili vumbi au takataka isiingie ndani.

Ndani ya sanduku ya nje kuna diski nyembamba au visahani moja, mbili au zaidi. Zinatengenezwa kwa kioo au aloi ya alumini. Diski hii imefunikwa kwa ganda la aloi lenye tabia ya kisumaku.

Kazi ya HDD

hariri

Kuandika

hariri

Diski inazungushwa kwa injini ya uememe ndogo haraka sana hadi mara 15,000 kwa dakika. Mkono unaoshika kalamu sumaku (huitwa pia "head" - kichwa) unapita juu yake. Kalamu unaacha alama sumaku kwenye mahali padogo usoni wa diski. Mfululizo wa nukta yenye chaji na nukta bila chaji inatunza habari kwa mfano herufi za alafabeti au pia picha. Chaji inabaki mahali pake kutokana na sifa za aloi inayofunika diski.

Kusoma

hariri

Wakati wa kusoma habari mkono unapita juu ya uso wa diski na kalamu inafanya kazi kinyume ya kuandika safari hii inagundua alama sumaku zilizopo na mfululizo wa nukta sumaku na nukta bila alama ya sumaku unasomwa na tarakilishi.

Kufuta

hariri

Wakati wa kufuta kumbukumbu mkono unapita juu ya sehemu ya diski ambako habari inatakiwa kufutwa na kuondoa chaji.

Kuna hatari ya kuweka sumaku karibu na kompyuta kwa sababu sumaku inaweza kuathiri kumbukumbu kwenye diski.