Djoser (majina mengine ni pamoja na Netjerikhet, Tosorthos, na Sesorthos) alikuwa Farao wa kwanza wa nasaba ya 3 ya Misri, mmamo mwaka 2670 KK. [1] Anakumbukwa kwa ujenzi wa piramidi ya kwanza iliyojengwa Misri ambayo ni piramidi ya ngazi huko Sakara. Nasaba ya Tatu iliyokuwa na mji mkuu wa Memphis, ilikuwa mwanzo wa Himaya ya Kale ya Misri na kipindi cha utulivu, mafanikio na umoja.

Sanamu ya Djoser katika Jumba la kumbukumbu la Misri mjini Kairo.

Kumbukumbu ya Djoser inaonyesha alitawala kwa miaka angalau miaka 20 lakini alitajwa kama mjenzi wa mahekalu mengi, makaburi na sanamu, hivyo wataalamu wengine wanasema inawezakana alitawala hata miaka 30.

Kuna sanamu ya rangi ya Djoser iliyochongwa na gange, ambayo ni ya kale kati ya sanamu za Kimisri zinazomwonyesha mtu kwa ukubwa wake halisi.[2] Iko sasa Jumba la kumbukumbu la Misri huko Kairo.

Piramidi ya Ngazi hariri

 
Piramidi ya ngazi huko Sakara.

Piramidi ya ngazi ya Djoser imetengenezwa kwa mawe ya gange. Msanifu aliyesimamia ujenzi wa piramidi hiyo aliku wa Imhotep, waziri wake na mtendaji mkuuwa farao. Ndani kuna chumba kidogo kinachofikiwa kwa ushoroba mwembamba. Kwenye chumba kulikuwa na mlango wa kuingia kwenye kaburi lililopo chini ya piramidi. Nafasi za ushoroba na chumba zilijazwa baadaye kwa chagarawe na udongo maana hazikuwa na kazi tena baada ya mazishi. Kiasili piramidi ilikuwa na kimo cha mita 62 kilichokaa juu ya msingi uliokuwa na vipimo vya mita 125 X 109. Uso wa nje ulikuwa gange iliyong'arishwa.

Marejeo hariri

  1. Ancient History Encyclopedia: Djoser - Ancient History Encyclopedia, accessdate: January 5, 2017
  2. King Djoser: The Egyptian Museum, Cairo, Egypt - King Djoser, accessdate: January 5, 2017