Dola la Roma Magharibi

Dola la Roma Magharibi ni sehemu ya Dola la Roma upande wa Magharibi iliyo na mji mkuu wa Roma. Kuanzia mwaka wa 285 Dola la Roma lilikuwa na makaisari wawili ili kurahisisha utawala wa en eneo lililokuwa kubwa mno.

Chini ya Konstantin Mkuu, mji wa Konstantinopoli ulitangazwa mji mkuu wa pili. Baada ya kifo cha Theodosius Mkuu, utawala uligawanywa kati ya wana wake na kweli kulikuwa na madola mawili yenye miji mikuu miwili.

Katika magharibi wanajeshi Wagermanik katika utumishi wa Waroma walipata uwezo zaidi hadi wakamua kushika madaraka wenyewe. Mtawala wa mwisho wa Roma Magharibi alikuwa Kaisari Romulus Augustus aliyeondoshwa madarakani mwaka wa 476. Mkuu wa jeshi Odoaker alimpindua Romulus akajitangaza kama mfalme wa magharibi hata akiendelea kuheshimu kipaumbele wa makaisari wa mashariki mjini Konstantinopoli.

Watawala Wagermanik wa Italia waliendelea kutawala katika jina la makaisari lakini hali halisi Dola la Roma Magharibi lilikuwa limekwisha.

Eneo la Dola la Roma Magharibi mwaka wa 395
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Dola la Roma Magharibi kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.