Dominic Bernard Patrick Monaghan (amezaliwa tar. 8 Desemba 1976) ni mwigizaji filamu wa Kiingereza. Amepata umaarufu kote duniani kwa kuigiza kama Meriadoc Brandybuck katika filamu ya The Lord of The Rings na pia kama Charlie Pace kwenye kipindi cha Lost. Hivi sasa, anaigiza kama Dr. Simon Campos kwenye kipindi cha FlashForward.

Dominic Monaghan

Amezaliwa Dominic Bernard Patrick Monaghan
Kazi yake Mwigizaji

Maisha yake hariri

Monaghan alizaliwa mjini Berlin, Ujerumani. Wazazi wake ni Maureen na Austin Monaghan, ambaye ni mwalimu wa sayansi.[1] Familia ya Monaghan waliishi katika miji ya Berlin, Dusseldorf-Lohausen, Stuttgart na Münster, wakihamahama kila takriban baada ya kila miaka minne. Baadaye, walihamia katika mji wa Manchester. Monaghan anaongea Kiingereza na Kijerumani vizuri.

Maisha ya kibinafsi hariri

Monaghan anapenda kupanda miti. Yeye anamiliki msitu mdogo nchini India na amefanya kazi kwenye tume za haki za wanyama kama PETA.[2] Monaghan anapenda wadudu, na amefuga wanyama kama kinyonga.[3]

Yeye anapenda kucheza kandanda na mpira wa kikapu. Yeye ni shabiki mkubwa wa timu ya Manchester United. Yeye anaishi mjini Los Angeles, California.

Yeye amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Evangeline Lilly ambaye ni mwigizaji mwenzake wa kipindi cha Lost kuanzia mwaka wa 2004. Mnamo Juni 2008, Monaghan alisafiri pamoja na Lilly mpaka nchi ya Argentina ili kurekodi filamu ya Caiga Quien Caiga.[4] Mnamo Juni 2009, yeye na Evangeline walisafiri pamoja kwenda Rwanda. Vilevile, wawili hawa wanaonekana pamoja mjini Vancouver.

Filamu hariri

Mwaka Filamu Aliigiza kama Maelezo
1997 Hostile Waters Sasha
2001 The Lord of the Rings: The Fellowship of the Ring Meriadoc Brandybuck
2002 The Lord of the Rings: The Two Towers Meriadoc Brandybuck
2003 The Lord of the Rings: The Return of the King Meriadoc Brandybuck Alishinda tuzo la Screen Actors Guild Award
An Insomniac's Nightmare Jack
2004 Spivs Goat
The Purifiers Sol
2005 Ringers: Lord of the Fans Mtangazaji
Shooting Livien Owen Scott
2008 I Sell The Dead Arthur Blake
2009 X-Men Origins: Wolverine Chris Bradley / Bolt
2011 Pet Seth

Vipindi hariri

Mwaka Kipindi Aliigiza kama Maelezo
1996 - 1998 Hetty Wainthropp Investigates Geoffrey Shawcross
2000 This is Personal: The Hunt for the Yorkshire Ripper Jimmy Furey
Monsignor Renard Etienne Pierre Rollinger
2004 - 2010 Lost Charlie Pace Mhusika mkuu tangu 2004 - 2007.
Alishinda tuzo la Screen Actors Guild Award.
2008 MADtv Mwenyewe Mnamo 26 Aprili 2008
2008 Caiga Quien Caiga Mwenyewe 23 Juni 2008. Pamoja na Evangeline Lilly
2009 Chuck Tyler Martin Kipindi kimoja
FlashForward Dkt. Simon Campos

Marejeo hariri

  1. Lost Boy. Jalada kutoka ya awali juu ya 2008-12-25. Iliwekwa mnamo 2010-01-28. Archived 25 Desemba 2008 at the Wayback Machine.
  2. Lost Star Dominic Monaghan Appears in New PETA Wildlife Ad. HelpingAnimals.com. Iliwekwa mnamo 21 Februari 2008.
  3. http://www.contactmusic.com/news.nsf/article/monaghan%20chameleon%20pets%20tearful%20goodbye_1032678
  4. Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2013-03-19. Iliwekwa mnamo 2010-01-28.

Viungo vya nje hariri