Dubai Gold Souk (Kiarabu: دبي سوق الذهب au Gold Souk) ni soko la jadi lililopo mjini Dubai. Soko hili lipo mjini mashariki mwa Dubai katika sehemu za biashara wilayani Deira. Kuna zaidi ya wauzaji 300 wanaofanya biashara. Kuna maduka ya rejareja katika soko hili yanayojulikana kama Damas, ARY jewellery, Prima Gold na Joy Allukas jewellery. Vilevile kuna maduka madogo madogo yanayojihusisha na biashara ya dhahabu pekee yake. Dubai Gold Souk iko katika maeneo ya Al Dhagaya. Kwa kutumia makadirio, takriban tani 10 za dhahabu hupatikana wakati wowote katika Souk [1]. Mipaka yake ya kaskazini ni Dubai Fish na Vegetable Market na Deira Corniche.

Dubai Gold Souk ina barabara nyembamba zilizopangwa na maduka mengi yanayouza dhahabu.
Duka moja la dhahabu iliyomo Gold Souk.


Biashara katika Soko hili la dhahabu iliimarishwa wakati wa miaka ya 1940 kutokana na mfumo wa Dubai wa kuruhusu biashara huria iliyovutia wanabiashara kutoka India na Iran kuanzisha maduka katika Soko hilo. Hata kama bei ya dhahabu ilizorota kote duniani katika soko la kimataifa, thamani ya biashara ya dhahabu na almasi kwa jumla njini Dubai, isiyo ya moja kwa moja na biashara ya mafuta, iliongezeka kutoka 18% mwaka 2003, hadi 24% mwaka 2004. Mwaka 2003, thamani ya biashara ya dhahabu mjini Dubai ilikadiriwa kuwa Dirhamu Bilioni 21 (dola bilioni 5.8), wakati biashara ya almasi ilikadiriwa kuwa Dirhamu Bilioni 25 (Dola bilioni 7) mwaka 2005. India ni mnunuzi mkubwa kabisa wa dhahabu, ikikadiria wastani wa 23% (2005) kwaa jumla ya dhahabu mjini Dubai katika biashara ya mwaka 2005. Uswisi ulikuwa msambazaji mkubwa wa dhahabu iliyomo Dubai. Vilevile, Bara Hindi ilikuwa na wastani wa 68% ya almasi yote inayohusiana na biashara mjini Dubai; Ubelgiji ikikadiriwa kuwa takriban ya 13% katika biashara ya almasi mjini Dubai (2005). [2]


Marejeo

hariri
  1. Dubai - City of Gold. Al Shindagha
  2. Dubai's trade in gold and diamonds continues to grow. Ilihifadhiwa 10 Februari 2012 kwenye Wayback Machine. Dubai's Chamber of Commerce and Industry.