Edwin Bruno Shayo (alizaliwa mkoani Kilimanjaro), ni mhandisi wa programu na mjasiriamali aliyeshinda tuzo. Ni mwanzilishi na mkurugenzi mtendaji wa Smart Codes Limited, kampuni ya teknolojia yenye makao yake makuu nchini Tanzania.

Ni mhitimu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph nchini Tanzania. Ubunifu wake wa M-Paper ilishinda tuzo ya Appsafrica.com ya uvumbuzi bora wa elimu mwaka wa 2015. Katika mwaka huo huo, Edwin Shayo alishinda Tuzo ya Chipukizi wa Vijana wakati wa Tuzo za Tanzania Leadership Awards. Mnamo mwaka 2016, jarida la Forbes lilimshirikisha katika orodha ya 30 chini ya 30 ya wajasiriamali wengi wenye ushawishi barani Afrika. [1].

Shayo alipata ladha yake ya kwanza ya ujasiriamali akiwa na umri wa miaka 13, akiuza kanda za muziki. Akiwa na miaka 17, alihamia kuuza CD. Akiwa chuo kikuu alitumia posho ya serikali ya kujikimu kwa kununua kompyuta yake ya kwanza. Akiwa na kiasi cha $10 pekee kama akiba, alichapisha kadi za biashara mbalimbali, alitengeneza tovuti za makampuni kutangaza bidhaa zao. Aliipa biashara jina la Smart Codes, wakala wa kidijitali ambao huangazia utangazaji, utafiti na uuzaji. Moja ya bidhaa zake zilizofanikiwa zaidi ni M-Paper, jukwaa ambalo husambaza magazeti na vitabu vilivyochapishwa moja kwa moja kwa simu za wasomaji. Smart Codes huingiza faida zaidi ya $350,000 kwa mwaka na ina wafanyikazi 29 wa kudumu na wafanyikazi 15 wa kandarasi. [2].

Marejeo

hariri
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Edwin Bruno kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.