Elsa Sjunneson

Mwandishi na Mhariri wa Marekani

Elsa Sjunneson (alizaliwa 1985[1]) ni mwandishi wa fasihi ya kubuni, mhariri, mkosoaji wa vyombo vya habari, na mwanaharakati wa haki za watu wenye ulemavu wa Marekani.

Ameshinda Tuzo za Hugo na Aurora kupitia kazi yake ya uhariri kwenye Jarida la Uncanny. Akiwa ni kiziwi na kipofu tangu kuzaliwa, Sjunneson anaandika na kuzungumza sana kuhusu uwakilishi wa watu wenye ulemavu katika utamaduni maarufu.

Wasifu

hariri

Elsa Sjunneson alizaliwa na ugonjwa wa congenital rubella syndrome, ambao ulisababisha kupoteza kusikia, mtoto wa jicho katika macho yote mawili, na tatizo la moyo.[2] Yeye ni kipofu kisheria na anatumia jicho la bandia pamoja na vifaa vya usaidizi wa kusikia pande zote mbili..[3]

Alisoma katika Chuo Kikuu cha Gonzaga, ambako alipata shahada ya kwanza ya historia mwaka 2008.[4][5] Akiwa Gonzaga, alifanya kazi ya kuhamasisha watu kuhusu FACE AIDS. Sjunneson aliendelea kusomea shahada ya uzamili ya historia ya wanawake kutoka Chuo cha Sarah Lawrence mwaka 2011

Marejeo

hariri
  1. "Sjunneson, Elsa, 1985-". Library of Congress Authorities. Iliwekwa mnamo Oktoba 27, 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Sjunneson-Henry, Elsa. "Rubella gave me a disability. This is my message to anti-vaxxers", CNN, February 19, 2019. (en) 
  3. Sjunneson-Henry, Elsa. "My artificial eye", Boston Globe, April 15, 2017. 
  4. "Elsa Sjunneson". Reedsy (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo Oktoba 27, 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "Alumni news from Gonzaga Magazine Spring 20". Gonzaga University (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo Oktoba 27, 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Elsa Sjunneson kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.