Epinastini (Epinastine), inayouzwa kwa jina la chapa Elestat miongoni mwa mengine, ni dawa inayotumika kutibu kuvimba kwa jicho kwa sababu ya mzio. Dawa hii inatumika kama tone la jicho.[1] Athari zake huanza ndani ya dakika tano na hudumu hadi masaa manane.[2] Dawa hii inaweza kutumika kwa hadi wiki nane.[3]

Epinastini
Jina la Utaratibu la (IUPAC)
(RS)-3-amino-9,13b-dihydro-1H-dibenz(c,f)imidazo(1,5-a)azepine
Data ya kikliniki
Majina ya kibiashara Alesion, Elestat, Purivist, Relestat
AHFS/Drugs.com Monograph
MedlinePlus a604011
Kategoria ya ujauzito C
Hali ya kisheria ?
Njia mbalimbali za matumizi Matone ya macho
Data ya utendakazi
Kufunga kwa protini 64%
Nusu uhai Masaa kumi na mbili
Vitambulisho
Nambari ya ATC ?
Visawe Epinastini hidrokloridi
Data ya kikemikali
Fomyula C16H15N3 
 YesY(Hiki ni nini?)  (thibitisha)

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kuwasha macho.[4] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha jicho kavu na mabadiliko ya ladha.[4] Dawa hii huzuia histamini na kudhibiti seli za mlingoti.[2] Haivuki kizuizi cha damu-ubongo.

Epinastini ilipewa hati miliki mwaka wa 1980, na ilianza kutumika kwa ajili ya matibabu mwaka wa 1994.[5] Nchini Uingereza mililita tano iligharimu Huduma ya Afya ya Kitaifa (NHS) takriban £10 kufikia mwaka wa 2021.[6] Kiasi hiki nchini Marekani kinagharimu takriban dola 31 za Kimarekani.[7]

Marejeo

hariri
  1. "Epinastine Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 1 Machi 2021. Iliwekwa mnamo 15 Desemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 "Epinastine Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 1 Machi 2021. Iliwekwa mnamo 15 Desemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)"Epinastine Monograph for Professionals". Drugs.com. Archived from the original on 1 March 2021. Retrieved 15 December 2021.
  3. BNF 81: March-September 2021. BMJ Group and the Pharmaceutical Press. 2021. uk. 1205. ISBN 978-0857114105.
  4. 4.0 4.1 BNF 81: March-September 2021. BMJ Group and the Pharmaceutical Press. 2021. uk. 1205. ISBN 978-0857114105.BNF 81: March-September 2021. BMJ Group and the Pharmaceutical Press. 2021. p. 1205. ISBN 978-0857114105.
  5. Fischer, Jnos; Ganellin, C. Robin (2006). Analogue-based Drug Discovery (kwa Kiingereza). John Wiley & Sons. uk. 549. ISBN 9783527607495. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-12-27. Iliwekwa mnamo 2021-03-08.
  6. BNF 81: March-September 2021. BMJ Group and the Pharmaceutical Press. 2021. uk. 1205. ISBN 978-0857114105.BNF 81: March-September 2021. BMJ Group and the Pharmaceutical Press. 2021. p. 1205. ISBN 978-0857114105.
  7. "Epinastine Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 8 Mei 2016. Iliwekwa mnamo 15 Desemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)