"Fallout" ni sehemu ya kumi na moja ya msimu wa kwanza wa mfululizo wa igizo la ubunifu wa kisayansi linalorushwa hewani na kituo cha televisheni cha NBC, Heroes.

"Fallout"
Sehemu ya Heroes

"Niambie, Claire, unaweza kutunza siri?"
Sehemu ya. Msimu 1
Sehemu 11
Imetungwa na Joe Pokaski
Imeongozwa na John Badham
Tayarisho la 111
Tarehe halisi ya kurushwa 4 Desemba 2006
Waigizaji wageni
Wendo wa sehemu
← Iliyopita Ijayo →
"Six Months Ago" "Godsend"
Orodha ya sehemu za Heroes

Hadithi

hariri

Sehemu inaanza na Mr. Bennet anamleta Claire nyumbani huku huku wakijadiliana kuhusu nguvu zake. Mr. Bennet anakubuli kwa Claire kwamba anajua kuhusu nguvu zake kabla hata yeye hajajua. Akawa na jazba naye, lakini kamtuliza kwa kumwambia alikuwa akijaribu kumlinda.

Anamwonya kwamba kuna watu wengine wabaya ambao watajaribu kumjeruhi iwapo watagundua kama ana nguvu za kipekee. Kisha anamwuliza nani mwingine anayefahamu kuhusu nguvu zake. Claire anamweleza kwamba Zach anajua yote kuhusu nguvu zake na ana uwezo gani, na Lyle naye amejua baadaya kuiba filamu za Claire akiruka kutoka juu ya kabisa ya mahali pa machimbo ya mafuta na kugongwa na gari.

Sylar amekamatwa na kushikiriwa kwenye selo ya kazini kwa Mr. Bennet. Mr. Bennet anamwambia Sylar kwamba nguvu zake hazitofanyakazi kwenye sehemu hii. Mr. Bennet anazungumza naye kuhusu nguvu zake kadha wa kadha ambazo anazitumia dhidi ya wenzake ambazo baadhi yao amezichukua. Sylar anajibu kwamba amepata hizo nguvu nyingine kwa sababu anajua vitu jinsi vinavyo "tiki", inamfanya kuwa wa kipekee kuliko wengine.

Mr. Bennet anamwabia Sylar kwamba huo ni uwendawazimu, kuwa na nguvu nyingi za DNA za kigeni na kupelekea kuharibu akili yake. Mr. Bennet anamwita Sylar kwa jina lake halisi, Gabriel, kitendo ambacho kimemkera vibaya sana - akajibamiza mwenyewe kwenye vioo na kupiga makelele, "My name is Sylar!" Mr. Bennet anamhabarisha kwamba atamegwa vipande-vipande na kuchambuliwa, akimfananisha na kitendo cha Sylar pindi anapokarabati saa zake, na kutambua kipi kinamfanya aweze "kutiki".

Viungo vya Nje

hariri