Fatma Juma Haji (alizaliwa Pemba, Zanzibar) ni mkufunzi wa umeme wa jua, pia ni meneja wa kituo cha umeme wa jua kiitwacho Barefoot kilichopo Kinyasini Kibokwa, Unguja. [1]

Elimu hariri

Fatma Juma Haji hakupata bahati ya kusoma mpaka mwaka 2011 alipochaguliwa kutoka kijijini Kandwi, Unguja kwenda India kujiunga na masomo ya umeme wa jua.

Baada ya masomo hayo yaliyodumu miezi sita, Fatma alirudi na kuajiriwa na chuo cha Barefoot[2] kama mkufunzi wa umeme wa jua, kazi kubwa ikiwa ni kufunga vifaa vya umeme wa jua katika vijiji tofauti visiwani Pemba na Unguja. Mpaka sasa Fatma Juma Haji ameweka vifaa vya umeme wa jua kwenye nyumba zaidi ya mia mbili visiwani humo.

Tofauti na visiwani, Fatma alikwenda pia nchi ya Sudan Kusini kusaidia wakufunzi wa umeme wa jua kufunga umeme katika vijiji mbalimbali nchini humo.

Fatma Juma Haji ameendelea kuweka nuru katika vijiji mbalimbali katika visiwa vya Unguja na Pemba. Pia amepata mialiko kutoka sehemu tofauti, alialikwa nchi ya Urusi kwa wiki mbili kufundisha akina mama tofauti kuhusu umeme wa jua.

Mwaka 2019 Fatma Juma Haji alipata mwaliko wa kuhudhuria nchini Ufaransa kuelezea kuhusu shughuli mbalimbali anazozifanya kuendeleza vijiji kwa kuwapa nuru ya umeme wa jua.

Marejeo hariri

  1. https://allafrica.com/stories/201209120402.html
  2. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-03-22. Iliwekwa mnamo 2020-04-07.