Fatou Jeng
Fatou Jeng ni mwanaharakati wa hali ya hewa wa vijana nchini Gambia, amelenga elimu, uhifadhi na upandaji miti . [1] [2] Anatambulika kimataifa kama mratibu wa hatua za hali ya hewa ya vijana nchini, pamoja na kuandaa Kongamano la Kitaifa la Vijana kuhusu Tabianchi, [1] [3] mratibu wa nchi na mjumbe wa bodi ya kimataifa ya Plant-for-the-Planet, [4] na shirika la Friday for Future. [5] Pia amehudumu kama msimamizi, mzungumzaji, na mtu wa rasilimali kwa programu kadhaa za kitaifa na kimataifa juu ya tabia nchi ikiwa ni pamoja na COP23 na COP24, Mkutano wa Global Landscapes wa 2018 wa Bonn, shirika la Action for Climate Empowerment 2018, na zaidi.
Jeng pia alianzisha shirika la vijana linaloongoza na lisilo la faida la Clean Earth Gambia. Lengo la shirika hilo ni kujenga uelewa kuhusu masuala ya mazingira, muhimu zaidi mabadiliko ya hali ya hewa. Pamoja na kufanya kazi ya kufundisha na kutoa mafunzo kwa zaidi ya watoto 500 wa shule kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa pamoja na masuala ya mazingira kwa jamii za wenyeji. [6]
Mnamo 2019, kwa UNFCC YOUNGO ya kwanza kabisa, ujumbe wa vijana kwenye Majadiliano ya Hali ya Hewa, alikuwa mmoja wa watu thelathini waliochaguliwa. Katika mkataba wa Umoja wa Mataifa alikuwa msukumo wa uwasilishaji wa sera kuhusu jinsia na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kiongozi wa uendeshaji wa sera kwa Wanawake na Jinsia. Pia mnamo 2019, alisaidia kuwezesha ushiriki wa vijana wakati wa wiki ya hali ya hewa ya Afrika. [7]
Alikuwa kijana bora kwa QTV Youth Dialogue Gambia Mwezi Juni 2019 kwa utetezi wake wa tabianchi, na kuelezewa na Whatson Gambia kama mmoja wa vijana 30 wa Gambia wenye ushawishi mkubwa. [8]
Mnamo 2021, Alitambuliwa kama mmoja wa Viongozi 100 wa Juu wa Uhifadhi wa Vijana wa Kiafrika na Muungano wa Afrika wa YMCAs, shirika la African Wildlife Fund, na mkusanyiko wa mashirika mengi ya kimataifa yasiyo ya faida.
Jeng alikuwa mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Gambia, na alikuwa rais wa kwanza mwanamke wa umoja wa wanafunzi wa chuo hicho. [8] [9] [10] Na kwa sasa anasoma katika Chuo Kikuu cha Sussex ambapo anafuata shahada yake ya uzamili katika mazingira, maendeleo, na sera.
Marejeleo
hariri- ↑ 1.0 1.1 "'We, too, want to be heard,' young African climate champions cry out". The East African (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-27. Iliwekwa mnamo 2020-08-26.
- ↑ "Fridays for Future: Can they keep the pressure up? | DW | 20.08.2020". DW.COM (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2020-08-26.
- ↑ "Gambian Young People Host Road to Nairobi Temperature Check with UNFPA Executive Director, Dr. Natalia Kanem". UNFPA Gambia (kwa Kiingereza). 2019-08-14. Iliwekwa mnamo 2020-08-26.
- ↑ "Gambian youth take the lead in tree planting initiatives". DIRAJ (kwa American English). 2020-06-05. Iliwekwa mnamo 2020-08-26.
- ↑ Foundation, Thomson Reuters. "We won't let your money destroy our future". news.trust.org. Iliwekwa mnamo 2020-08-26.
{{cite web}}
:|first=
has generic name (help) - ↑ "Meet the eight African women shaping the future of the continent". Landscape News (kwa American English). 2021-05-25. Iliwekwa mnamo 2021-06-20.
- ↑ "Know More About The First Female President Of The University of the Gambia. | Afrinity Productions" (kwa American English). 2020-10-07. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-02-27. Iliwekwa mnamo 2023-02-27.
- ↑ 8.0 8.1 Saja. "The 30 most influential young Gambians of 2019". www.whatson-gambia.com (kwa Kiingereza (Uingereza)). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-10-31. Iliwekwa mnamo 2020-08-26.
- ↑ "Gambian Women: Role models for fruitful and equal opportunities | Commonwealth Scholarship Commission in the UK" (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-04-08. Iliwekwa mnamo 2020-08-26.
- ↑ "UTG Elects 1st Female President". The Digest (kwa American English). 2018-03-30. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-11-14. Iliwekwa mnamo 2020-08-26.