Filamu za Hood

(Elekezwa kutoka Filamu ya hood)

Filamu za Hood (kutoka Kiingereza: Hood film) ni aina ya filamu yenye asili ya Marekani hasa mwishoni mwa miaka ya 1980 na mwanzoni mwa miaka ya 1990. Ndani yake mna hasa mambo ya mjini kama vile muziki wa hip hop, wahuni wa mtaani, ubaguzi wa rangi, umaskini, na matatizo ya Wamarekani Weusi hasa vijana jinsi wanavyopata shida na jamii ya Kizungu. Filamu za namna hiyo huhusisha hasa waigizaji wa Kiafrika-Kiamerika.

Mfano halisi wa filamu za aina hii ni kama vile Boyz n the Hood na Menace II Society, ambazo mtindo wake wa hadithi almanusura iupe umaarufu kupindukia mchezo huu. Mwanzoni mwa miaka ya 1996, lakini, filamu za Hood zilionekana kama chombo cha watengenezaji filamu weusi kinachohaha kukwepa tofuati bayana ya ufananisho wa filamu za Kizungu. Mtindo huu pia ulikuja kugezewa tena na filamu kama vile Don't Be a Menace to South Central While Drinking Your Juice in the Hood.

Filamu za Kiingereza za mtindo huu nazo zilipata kufanywa, kama vile Bullet Boy. Filamu za Kifaranza za mtindo huo nazo zimefanya, La Haine, Ma 6-T va crack-er, Yamakasi na Banlieue 13 nazo ni mifano ya mtindo huu.

John Singleton, Mario Van Peebles, Hughes Brothers, na Spike Lee ni mifano tosha ya waongozaji wa filamu za namna hii.

Insha kadha wa kadha ziliandikwa kuhusu mtindo huu na Paula J. Massood, ambaye kwa sasa ni mwalimu katika Brooklyn College.[1]

Mwaka wa 1992 insha kuhusu masuala ya uigizaji wa sinema, mchambuzi wa Kikanada Rinaldo Walcott amegundua msingi wa filamu za Hood ni kutaka kuonesha ujanadume, au kurudisha heshima ya utu wa mtu mweusi".[2]

Orodha ya filamu za Hood hariri

Marejeo hariri

  1. Murray Forman (2002). The 'Hood Comes First: race, space, and place in rap and hip-hop. Wesleyan University Press. 
  2. John McCullough (2006). "Rude and the Representation of Class Relations in Canadian Film". Working on Screen: Representations of the Working Class in Canadian Cinema. University of Toronto Press. 

Vyanzo hariri

  Makala hii kuhusu filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Filamu za Hood kama waigizaji wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.