Flamenco
Flamenco ni jina la aina ya muziki na dansi katika utamaduni wa Hispania.
Inajumlisha
- uimbaji (his. cante)
- muziki ya ala (his. toque), hasa gitaa
- dansi
Tangu mwaka 2010 Flamenco inahesabiwa kati ya urithi wa dunia.
Sehemu ya uimbaji ni pia upiga wizani. Hapo kuna njia mbalimbali: kwa makofi, kwa miguu, kwa kupiga ala kama ngoma, kwa kastaneti ambazo ni vipande vya ubao vinavyofungwa kwenye vidole.
Sehemu ya ndani mara nyingi ni mwanaume mmoja na mwanamke mmoja mbele ya watazamaji, isipokuwa kuna pia makundi ya wachezaji dansi mbele ya watazamaji wanaounga katika kupiga wizani.