Yosefu Flavius
Yosefu Flavius (jina la awali יוסף בן מתתיהו, Yosef bin Matityahu, 37-100 BK) alikuwa kuhani Myahudi mwenye kujua Kiaramu, Kiebrania na Kigiriki, aliyejipatia umaarufu kama mwanahistoria.
Maisha
haririKwanza alishiriki vita vya ukombozi vya Wayahudi dhidi ya Warumi akishika nafasi ya uongozi huko Galilaya.
Mwaka 67 alisalimu amri akawa mtumwa na mkalimani wa Vespasian kwa miaka miwili.
Huyo alipopata kuwa kaisari alimuacha huru, naye akajiongezea jina Flavius la ukoo wa Vespasian.[1]
Alipata uraia wa Roma, akawa mshauri na mkalimani wa Tito, mwana wa Vespasian, wakati wa kushambulia na hatimaye kuteka Yerusalemu (70).
Maandishi
haririVitabu vyake muhimu zaidi vinaitwa kwa Kiingereza The Jewish War (75 hivi) na Antiquities of the Jews (94 hivi).[2]
Cha kwanza kinasimulia vita vya kwanza vya Wayahudi dhidi ya Roma (66-73).
Cha pili kinasimulia historia ya ulimwengu kwa mtazamo wa Kiyahudi lakini namna inayoweza kukubaliwa na Warumi.
Maandishi hayo ni muhimu katika kuelewa Uyahudi wa karne ya 1 na mwanzo wa Ukristo.[2]
Tanbihi
hariri- ↑ Simon Claude Mimouni, Le Judaïsme ancien du VIe siècle avant notre ère au IIIe siècle de notre ère : Des prêtres aux rabbins, Paris, P.U.F., coll. « Nouvelle Clio », 2012, pag. 133.
- ↑ 2.0 2.1 Stephen L. Harris, Understanding the Bible, (Palo Alto: Mayfield, 1985).
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Yosefu Flavius kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |