Forodha (ing. customs) ni jina la mamlaka ya nchi inayosimamia kuingia na kutoka kwa bidhaa zikivuka mipaka. Tangu kale kazi yake ni hasa kukagua thamani ya bidhaa na kudai malipo ya ushuru[1] ambayo ni pesa inayokadiriwa kama sehemu ya thamani ya bidhaa kwa kibali cha kuzileta au kuzitoa nchini.[2]

Nembo la kimataifa la forodha
Afisa na mbwa wa forodha wakikagua mzigo kwenye uwanja wa ndege

Kwa hiyo vituo vya forodha hupatikana kwenye mpaka wa nchi, pamoja na bandarini, uwanja wa ndege na ofisi za posta kwa vifurushi kutoka nje.

Kazi muhimu ya forodha ni pia kudhibiti bidhaa haramu kama madawa ya kulevya au bidhaa hatari ambako ni lazima kuhakikisha zinasafirishwa kwa njia salama, pamoja na hati zinazoonyesha maudhui yake kikamilifu.

Nchini Tanzania forodha ni sehemu ya Mamlaka ya Mapato ya Tanzania chini ya kamishna wa ushuru wa forodha na bidhaa.

Marejeo

hariri
  1. "Forodha", Kamusi Kuu ya Kiswahili, Baraza la Kiswahili la Taifa 2015
  2. Linganisha Biashara ya kuvuka mipaka, tovuti ya TRA, iliangaliwa Machi 2023

Viungo vya Nje

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Forodha kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.