Fufu (Chakula)

(Elekezwa kutoka Foufou)

Fufu (majina mengine ni pamoja na foofoo, foufou, foutou) ni chakula kikuu cha Afrika ya Magharibi na Afrika ya Kati. Ni ugali mnene ambao kwa kawaida huandaliwa kwa kuchemsha unga/Wanga (utokanao na mihogo, viazi vikuu, magimbi) katika maji na kupondwapondwa mpaka hali inayotakiwa ifikiwe. Katika mataifa ya Afrika ya Magharibi yanayozungumza Kifaransa kama Kamerun, fufu wakati mwingine unajulikana kama couscous (couscous de Cameroun ), chakula hiki hakina uhusiano wowote na mlo wa Kimoroko wa couscous.

Sahani ya fufu pamoja na supu ya njugu

Katika eneo la Afrika ya Magharibi, fufu kwa kawaida huandaliwa kutoka kwa mihogo, viazi vikuu na wakati mwingine huchanganishwa na viazi vikuu vya coco, plantain(mmea katika jamii ya ndizi) au mahindi. Nchini Ghana, fufu mara nyingi huandaliwa kutoka kwa mihogo iliyochemshwa na plantain bichi zilizopigwa pamoja, pamoja na kutoka kwa viazi vikuu vya coco. Hivi sasa, bidhaa hizi zimebadilishwa kuwa poda / unga na zinaweza kuchanganywa na maji ya moto kupata bidhaa ya mwisho hivyo basi kuondoa kazi ngumu ya kuipondaponda Katika Afrika ya Kati na nchi ya Liberia, fufu mara nyingi huandaliwa kutoka kwa mihogo. Fufu pia inaweza kuandalia kutoka kwa semolina (nafaka ya ngano), mchele, au hata vipande vya viazi. Mara nyingi, mlo huu bado huandaliwa kutumia mbinu za kitamaduni: kupondaponda na kupiga msingi wa dutu kutumia kijiko wa mbao. Katika muktadha ambazo umaskini siyo hoja au ambapo mitambo ya kisasa hupatikana kwa urahisi, mashine ya usindikaji wa chakula pia inaweza kutumika.

Mizizi ya mihogo inakaushwa, kisha inapoondwa kuwa unga na kuongezwa kiwango cha maji ili kuifanya iwe "luku" katika Mkoa wa Bandundu, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Katika Afrika ya Magharibi na Afrika ya Kati, mbinu inayotumika kwa kawaida ni kupakua mlima wa fufu pamoja na supu lililiandaliwa kutoka kwa kisamvu(okra), samaki (mara nyingi hukaushwa), nyanya, nk Nchini Ghana, fufu huliwa na supu ya nyanya ambayo si nene, supu ya mitende, supu ya njugu au aina zingine za supu za mboga kama vile nkontomire (majani ya viazi vikuu vya coco). Supu mara nyingi huandaliwa kutuimia aina mbalimbali ya nyama na samaki, freshi au iliyowekwa kwa moshi. Mlaji huchuna mipira ndogondogo ya fufu na hutengeneza shimo kwa mipira hiyo kutumia kidole cha gumba. Hifadhi au shimo hii kisha hujazwa na supu, na mpira hii huliwa. Nchini Ghana na Nigeria, mpira huu mara nyingi huwa hautafunwi bali humezwa mzima. Kwa kweli, kutafuna fufu ni kosa la aibu,amini usiamini!

Faili:FuFu flour.jpg
Packages ya unga fufu kuuzwa katika soko Los Angeles

Chakula kingine kuu katika Sub-Sahara ya Afrika sawa na fufu ni Ugali, ambayo kwa kawaida huandaliwa kutoka kwa unga wa mahindi na huliwa katika kusini na mashariki ya Afrika. Jina Ugali ni linatumika nchini Kenya na Tanzania; chakula kingine kinachohusiana na ugali kwa karibu kinajulikana kama nshima nchini Zambia, nsima nchini Malawi, sadza nchini Zimbabwe, pap nchini Afrika Kusini, posho nchini Uganda, luku, fufu, nshima, moteke na bugari katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Nchini Nigeria rangi ya fufu ni nyeupe na imeshikana. Mbinu ya kitamaduni ya kula fufu ni kuosha mikono yako kisha kuchukua mpira wa fufu wenye ukubwa wa mawe ndogo kutumia mkono wa kulia. Kisha mlaji anatengeneza shimo ndogo katika mpira na kuchota kitoweo au supu alionao; hatimaye kula fufu yenyewe. Kwa hivyo Fufu haitumiki tu kama chakula lakini pia kama chombo cha kula!

Neno Foo-foo limetajwa mara nyingi katika kitabu/tamthilia(novel) ya Chinua Achebe, Things Fall Apart.

Fufu ya Karibi

hariri

Katika mataifa ya Karibi yenye wakazi wa asili ya Afrika ya Magharibi, kama Kuba, Jamhuri ya Dominika na Puerto Rico, plantains ni hupondwa na kisha viungo vingine huongezwa. Nchini Kuba hiyo inaitwa fufu de platano. Katika Jamhuri ya Dominika na Puerto Rico mlo huu unajulikana kama mangu na mofongo, mtawalia. Tofauti kati ya fufu ya Afrika na fufu ya Caribbean hubainishwa katika unyororo na ladha, fufu ya Caribbean na mofongo sanasana ni kama ugali bali si kama uji.

Asili ya Fufu ni Ghana na raia wa Ghana wanalitamka neno hili kama fufuo. Neno fufu liliibuka kutoka lugha ya Kighana (twi). Fufu huliwa na supu ya li, supu ya njugu uliosagwa na supu ya inquatiquine.

Marejeo

hariri

Angalia pia

hariri
  • EBA
  • Mangu
  • Mofongo
  • Mlo wa unga wa mahindi
  • Couscous
  • Polenta
  • Poi
  • Viazi vilivyopondwa
  • Mămăliga
  • Ugali
  • Bazeen

Viungo vya nje

hariri
 
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fufu (Chakula) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.