Francis Coquelin

Mchezaji mpira wa Ufaransa

Francis Coquelin (alizaliwa 13 Mei 1991) ni mchezaji wa Ufaransa ambaye huchezea klabu ya Arsenal kama mchezaji wa kati. Yeye alijiunga na klabu ya Arsenal kutoka Stade Lavallois katika majira ya joto ya mwaka wa 2008.

Francis Coquelin
Maelezo binafsi
Jina kamili Francis Coquelin
Tarehe ya kuzaliwa 13 Mei 1991
Mahala pa kuzaliwa    Laval,Mayenne, Ufaransa
Urefu 1.78m
Nafasi anayochezea Mchezaji wa kati
Maelezo ya klabu
Klabu ya sasa Valencia C.F.
Namba 35
Klabu za vijana
2000-2005
2005-2008
2008
AS du Bourny
Stade Lavallois
Arsenal
Klabu za ukubwani
Miaka Klabu
2008-2018 Arsenal
Timu ya taifa
2007-2008
2008-2009
2009
Ufaransa-Vijana walio chini ya umri wa miaka 17
Ufaransa-Vijana walio chini ya umri wa miaka 18
Ufaransa-Vijana walio chini ya umri wa miaka 19

* Magoli alioshinda

Wasifu wa Klabu hariri

Aliyezaliwa Laval, Mayenne, Coquelin alianza kwa kuchezea timu ya As Laval Bourny kabla ya kutoka timu hiyo katika mwaka wa 2005 akihamia klabu kubwa kabisa katika eneo hilo,Stade Lavallois. Coquelin alicheza katika klabu hiyo hadi talanta yake iliponekana na skauti wa wachezaji wa Arsenal, Gilles Grimandi. Talanta yake ilionekana katika Shindano la UEFA la Uropa la vijana waliokuwa chini ya miaka 17 la 2008 walipokuwa wakicheza dhidi ya Israeli.

Arsenal hariri

Msimu wa 2008/09 hariri

Mnamo Julai 2008, Coquelin alijiunga na Arsenal kutoka Stade Lavallois kufuatia mafanikio katika majaribio yake na klabu. Ingawa alipata jeraha la paja lililosimamisha majaribio yake,alikuwa amewavutia wataalam wa Arsenal na akapewa mkataba na klabu. Coquelin alicheza kwa mara ya kwanza katika timu ya Arsenal alipocheza katika mechi ya kabla msimu dhidi ya Barnet na Szombathelyi Haladas na akacheza mechi yake ya kwanza kubwa kwa timu hiyo katika ushindi wao dhidi ya timu ya Sheffield United mnamo 23 Septemba 2008.Aliingia kama mchezaji mbadala kwa Fran Merida na kucheza kama difenda katika mechi hiyo waliyoshinda 6-0. Coquelin alifunga bao lake la kwanza kama mchezaji wa Arsenal katika mechi ya timu hifadhi dhidi ya Stoke City mnamo 6 Oktoba 2008 kwa mkwaju wa nguvu na mguu wake wa kushoto.

Msimu wa 2009/10 hariri

Coquelin alianza katika timu ya kwanza alipocheza katika mechi dhidi ya West Bromwich Albion Shindano la Kombe la League,akicheza dakika 58 kabla ya kubadilishwa na Mark Randall kuanza kufanywa kwanza kwa timu ya kwanza dhidi ya West Bromwich Albion katika Duru ya tatu ya Kombe la Ligi, kucheza dakika 58 kabla ya yeye ersattes Mark Randall.

Mtindo wa kucheza hariri

Amesifika kama mchezaji mwenye kunyang'anya mpira kwa njia ya nguvu lakini halali.Amefananishwa na Claude Makelele na Lassana Diarra kwa kuwa mdogo lakini mwenye roho.

Tuzo hariri

Arsenal hariri

  • Kombe la Vijana La FA: 2009
  • Ligi ya FA ya Shule: 2009

Takwimu ya Wasifu hariri

(sahihi tangu 28 Oktoba 2009)
Klabu Msimu Ligi Kombe la FA Kombe la Carling Uropa Total
Mechi alizocheza Mabao Usaidizi katika kufunga bao Mechi alizocheza Mabao Usaidizi katika kufunga bao Mechi alizocheza Mabao Usaidizi katika kufunga bao Mechi alizocheza Mabao Usaidizi katika kufunga bao Mechi alizocheza Mabao Usaidizi katika kufunga bao
Arsenal 2008–09 0 0 0 0 0 0 1 0 0 0 0 0 1 0 0
Arsenal 2009–10 0 0 0 0 0 0 2 0 0 0 0 0 2 0 0
Jumla 0 0 0 0 0 0 3 0 0 0 0 0 3 0 0

Marejeo hariri

Viungo vya nje hariri