Freestyle Football Tanzania
Freestyle Football Tanzania Association ni chombo cha mchezo wa uchezeaji wa mpira wa miguu (uchezea mpira) nchini Tanzania kama vile serikali ama shirikisho linavyofanya shughuli zake.
FFTA inasimamiwa na kuendeshwa na mfumo wa utawala wa klabu moja iitwayo Genius MP Freestyle Football Club. Klabu hii ni klabu mama ya mchezo huu yenye jukumu na mamlaka ya kusimamia, kuendesha, na kuratibu mchezo huu nchini na ndio inayotoa viongozi wakutawala FFTA. Klabu ina usajili wa namba NSC 11410 (National Sports Council). FFTA inahusiana na shirikisho la dunia la uchezeaji mpira wa miguu (World Freestyle Football Federation-WF3) [1] ambalo balozi wake mkuu ni Ronaldinho.
Historia ya FFTA
haririFFTA kabla ya kuwa chombo kilikuwa kinatambulika kama Chama cha uchezeaji wa mpira wa miguu wa Tanzania - TFFA (Tanzania Freestyle Football Association) [2], hivyo kilijulikana rasmi na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mnamo Julai 19, 2015 kama FFT (Freestyle Football Tanzania) kupitia wizara ya michezo na baraza la michezo.[3]. FFT iliweza kusajili klabu ya kwanza iitwayo Genius MP. Morison Mosses Jumanne [4] ndiye rais wa awamu ya I ya FFT na mwenyekiti wa klabu ngazi ya taifa na Pascal Chang'a ndiye makamu wa rais wa awamu ya I ya FFT na makamu mwenyekiti wa klabu ngazi ya taifa tangu Julai 19, 2015.
Klabu ya Genius MP
haririNi klabu mama ya mchezo wa kuchezea mpira wa miguu yenye jukumu na mamlaka ya kusimamia, kuendesha na kuratibu mchezo huu. Ilianzishwa 2015 na kusajiliwa Aprili 27, 2016 kwa kupewa namba ya usajili NSC 11410. Klabu ina uhusiano na shirikisho la ulimwengu ambalo balozi wake mkuu ni Ronaldinho Gaucho. Waanzilishi ni Morison Mosses Jumanne na Pascal Chang’a.
Ujio wa bingwa wa uchezeaji mpira wa miguu duniani mwaka 2012, Kotaro Tokura
haririKotaro Tokura ni raia wa Japan. Ni mchezaji wa kuchezea mpira wa miguu, alishiriki shindano la dunia mwaka 2012 na alifanikiwa kuwa mshindi wa kwanza wa dunia.
Madhumuni ya FFT
hariri(a) Kupiga vita aina zote za ukatili wa kijinsia na uvunjaji wa haki za wachezeaji mpira.
(b) Uwepo wa mashindano ya kata, wilaya, kanda, mkoa, kitaifa na mataifa na ya mashirika ya umma na binafsi.
(c) Kujenga uwezo kwa kutoa elimu katika masuala ya elimu ya mchezo.
(d) Kutetea na kushawishi uboreshaji wa miundo mbinu na huduma za mchezo katika ngazi mbalimbali.
(e) Kuwezesha upatikanaji wa fursa mbalimbali za kimaendeleo na kushawishi wachezeaji kujiunga katika vikundi mitandao mbalimbali yenye manufaa kwa wachezeaji.
(f) Kuhakikisha ukuaji wa soko la mchezo linakuwa kubwa.
(g) Kuifanya sekta ya michezo kukua kiuchumi.
(h) Kuwepo kwa ajira kwa waendeshaji na wachezeaji mpira.
Mashindano ya FFT
hariri1.Ya Ndani – Tanzania [5]
2.Ya Nje – Afrika na Mabara[6]
3.Mengine[7]
Tanbihi
hariri- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-05-03. Iliwekwa mnamo 2021-01-16.
- ↑ kilidumu kwa muda wa miezi kadhaa kuanzia Aprili 25, mwaka 2015 hadi Julai 19, 2015
- ↑ FFT ilianzishwa na Morison Mosses Jumanne na Pascal Chang'a.
- ↑ https://www.instagram.com/morisonmosses/
- ↑
- KiTaifa – Tanzanian Freestyle Football Championship
- KiKanda - Zonal Freesyle Football Championship
- KiMkoa – Region Freestyle Football Championship
- KiWilaya - District Freestyle Football Championship
- KiKata – Ward Freestyle Football Championship
- ↑
- Afrika Mashariki – East African Freestyle Football Championship
- Afrika – African Freestyle Football Championship
- Supeball – World Open Freestyle Football Championship
- Dunia – World Freestyle Football Campionship
- Tour – World Freestyle Football Tour
- ↑
- Ya matukio (Ndondo Cup, n.k)
- Kampuni / Taasis (RedBull, Airtel, Tigo, Cocacola n.k)