Freetown ni mji mkuu pamoja na bandari kubwa na kitovu cha uchumi wa nchi ya Sierra Leone. Uko kando ya Atlantiki kwenye rasi ya Freetown. Idadi ya wakazi ni 1,070,000.

Jiji la Freetown
Nchi Sierra Leone
Muonekano wa Mji wa Freetown

Historia

hariri

Mji uliundwa mwaka 1787 kwa ajili ya watumwa wenye asili ya Afrika waliowekwa huru. Ndiyo asili ya jina "Freetown" linalomaanisha "Mji wa watu huru".

Ulikuwa mji mkuu wa koloni la Uingereza katika Afrika ya Magharibi kati ya miaka 1808 hadi 1874.

Hadi leo Wakreoli ambao ni wazao wa watumwa waliopewa uhuru kama walowezi ni tabaka la pekee Freetown wakionekana kwa utamaduni na lugha ya pekee.

Katika miaka ya 1990 mji ulikuwa mahali pa mapigano kati ya wanamgambo na askari za ECOWAS.

Uchumi

hariri

Uchumi wa Freetown unategemea hasa bandari. Kuna pia viwanda vya sigara, vya kutengeneza petroli, vya chakula na za kusafisha almasi.

Tazama pia

hariri
  Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Freetown kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.