Fur Elise
"Für Elise" (maana yake: Kwa ajili ya Elise) ni jina la kutaja ala maarufu iliyopigwa katika mtindo "Bagatelle katika A minor". Mtunzi wa kibwagizo hiki ni hayati Ludwig van Beethoven kutoka nchini Ujerumani. Alitunga kibwagizo hiki mnamo mwaka wa 1810. Muziki kwa ajili ya piano pekee. "Für Elise" ni moja kati ya vibwagizo vya piano maarufu duniani. Wapiga piano wengi wanataka kujifunza namna ya kupiga kibwagizo hiki.
Therese Malfatti: "Für Elise" huenda ikawa iliandikwa kwa ajili yake.
|
|
Problems listening to this file? See media help. |
Hakuna anayefahamu Elise alikuwa nani. Inawezekana alikuwa mwanamama mmoja aliyeitwa Therese ambaye Beethoven alitaka kumuoa mnamo 1810. Lakini Therese hajataka kuolewa naye. Kibwagizo hiki hakijachapishwa hadi mwaka wa 1865, kitambo sana tangu kifo cha Beethoven.
Kibwagizo hiki kipo katika muundo wa rondo. Kuna kipengele kikuu cha (A) ambacho kinaonekana mara tatu. Kati ya hizi sehemu tatu kuna vileviel sehemu nyingine mbili (B na C), hivyo basi muundo wa kibwagizo hiki kinaweza kuelezewa kama: A B A C A.
Kipenge au sehemu kuu ina alama ya muda wa 3/8. Ipo katika msingi wa arpeggio ambayo inatambaa kutoka mkono mmoja hadi mwingine. Hiki ni kipengele ambacho watu wengi wanaoanza kujifunza upigaji piano wanapenda kukipiga. Vipinge vya pili ambavyo vipo kati ni vigumu sana kuvipiga katika mwendo sahihi. Ina jamii ya sauti (scale) inayoenda kasi sana, arpeggio na mkono wa kushoto ni demisemiquavers (nota 32).
Marejeo
hariri- Woodstra, Chris. et al. 2005. All Music Guide to Classical Music. All Media Guide, LLC. p. 104. ISBN 0-87930-865-6
- Klaus Martin Kopitz, Beethoven’s ‘Elise’ Elisabeth Röckel: a forgotten love story and a famous piano piece, in: The Musical Times, vol. 161, no. 1953 (Winter 2020), pp. 9–26 klaus-martin-kopitz.de (PDF)
Viungo vya Nje
hariri- Für Elise - and other Beethoven resources (includes the free sheet music)
Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Fur Elise kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |