Fyekeo

Zana za Kilimo

Fyekeo[1] (kutoka kitenzi "kufyeka"; kwa Kiingereza scythe) ni zana ya kilimo kwa ajili ya kukata nyasi au nafaka kama ngano. Muundo wake unafanana na mundu lakini kisu na mpini ni mrefu zaidi. Zinamwezesha mtumiaji kukata eneo kubwa kwa urahisi kulinganishwa na matumizi ya mundu au kifyekeo cha kawaida.

Fyekeo na mundu.
Mchoro ukionyesha mkulima anayetumia fyekeo.

Mtumiaji wake anasimama wakati anakata nyasi. Kisu kinahitaji kunolewa mara kwa mara, hivyo kila mtumiaji hubeba pia jiwe la kunoa.

Fyekeo ilikuwa kifaa kikuu cha kukata nyasi na kuvuna nafaka katika Ulaya, Asia ya Magharibi na Marekani hadi kusambaa kwa mashine zinazotekeleza shughuli hizo. Fyekeo zinatumiwa bado, hasa katika mazingira ambako tabia ya uso wa ardhi hairuhusu matumizi ya mashine.

Katika Afrika matumizi ya fyekeo hayajaenea; inasemekana mara nyingi nyasi za Afrika ni ngumu mno kwa zana hiyo. Hata hivyo kuna majaribio ya kufundisha matumizi yake kwa wakulima wadogo wasio na uwezo wa kugharamia mashine[2].

Katika Kiswahili neno fyekeo linatumika zaidi kumaanisha "kwanja".

Tazama pia hariri

Marejeo hariri

  1. Makala inatumia istilahi "fyekeo" kwa zana hiyo kama majaribio; tunafuata kamusi ya TUKI-ESD uk. 789
  2. A holistic introduction of scythes into Africa; an example, Big Book of the Scythe, Part 3

Tovuti za Nje hariri

Video hariri