Gabapentini (Gabapentin), inayouzwa kwa jina la chapa Neurontin miongoni mwa mengineyo, ni dawa ya kuzuia mshtuko inayotumika kutibu mishtuko kiasi ya moyo, maumivu ya neva, kuwaka moto, na ugonjwa wa miguu isiyotulia.[1] [2] Inapendekezwa kama mojawapo ya idadi ya dawa za mstari wa kwanza kwa ajili ya kutibu maumivu ya neva yanayosababishwa na ugonjwa wa neva wa kisukari, maumivu yanayotokea karibu na kwenye eneo ambalo upele uliwahi kuwa, na maumivu ya neva ya kati.[3] Takriban 15% ya watu walio na ugonjwa wa neva wa kisukari, maumivu yanayotokea karibu na kwenye eneo ambalo upele uliwahi kuwa wana faida inayoweza kupimika. Gabapentini inachukuliwa kupitia njia ya mdomo.[1]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na usingizi mwingi na kizunguzungu.[1] Madhara yake makubwa ni pamoja na kuongezeka kwa hatari ya kujiua, tabia ya uchokozi, na athari za dawa za kulevya.[1] Haijulikani ikiwa ni salama wakati wa ujauzito au kunyonyesha.[4] Vipimo vya chini vinapendekezwa katika utendakazi wa chini wa figo.[1] Gabapentini ni dawa ya kundi la kuzuia kifafa ambayo hutumiwa sana kutibu maumivu ya ugonjwa wa neva.[5] Ina muundo wa molekuli sawa na ule wa γ-asidi ya aminobutiriki (GABA) ya kemikali asilia zinazoruhusu niuroni kuwasiliana katika mwili wote na hufanya kazi kwa kuzuia baadhi ya njia za kalsiamu.[6][5][7]

Gabapentini iliidhinishwa kwa mara ya kwanza kutumika mwaka wa 1993.[8] Imekuwa ikipatikana kama dawa ya kawaida nchini Marekani tangu mwaka wa 2004.[1] Bei yake ya jumla katika ulimwengu unaoendelea kufikia mwaka wa 2015 ilikuwa takriban US$10.80 kwa mwezi;[9] na nchini Marekani, ilikuwa US$100 hadi US$200.[10] Mnamo mwaka wa 2017, ilikuwa dawa ya kumi na moja inayoagizwa zaidi nchini Marekani, ikiwa na maagizo zaidi ya milioni 46.[11][12] Katika miaka ya 1990, Parke-Davis, kampuni tanzu ya Pfizer, ilianza kutumia mbinu kadhaa haramu kuwahimiza madaktari nchini Marekani kutumia gabapentini kwa matumizi ambayo hayajaidhinishwa.[13] Wamelipa mamilioni ya dola kutatua kesi mbalimbali kuhusu shughuli hizi.

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 "Gabapentin". The American Society of Health-System Pharmacists. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 19 Agosti 2017. Iliwekwa mnamo 23 Okt 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Wijemanne S, Jankovic J (Juni 2015). "Restless legs syndrome: clinical presentation diagnosis and treatment". Sleep Medicine. 16 (6): 678–90. doi:10.1016/j.sleep.2015.03.002. PMID 25979181.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. Attal N, Cruccu G, Baron R, Haanpää M, Hansson P, Jensen TS, Nurmikko T (Septemba 2010). "EFNS guidelines on the pharmacological treatment of neuropathic pain: 2010 revision". European Journal of Neurology. 17 (9): 1113–e88. doi:10.1111/j.1468-1331.2010.02999.x. PMID 20402746.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Gabapentin Pregnancy and Breastfeeding Warnings". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 29 Agosti 2017. Iliwekwa mnamo 13 Machi 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. 5.0 5.1 Calandre EP, Rico-Villademoros F, Slim M (Novemba 2016). "2delta ligands, gabapentin, pregabalin and mirogabalin: a review of their clinical pharmacology and therapeutic use". Expert Review of Neurotherapeutics. 16 (11): 1263–1277. doi:10.1080/14737175.2016.1202764. PMID 27345098.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. Sneader, Walter (2005). Drug Discovery: A History. John Wiley & Sons. ku. 219–220. ISBN 978-0-470-01552-0. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 8 Septemba 2017. Iliwekwa mnamo 31 Agosti 2017.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. Uchitel OD, Di Guilmi MN, Urbano FJ, Gonzalez-Inchauspe C (2010). "Acute modulation of calcium currents and synaptic transmission by gabapentinoids". Channels. 4 (6): 490–6. doi:10.4161/chan.4.6.12864. PMID 21150315.
  8. Pitkänen, Asla; Schwartzkroin, Philip A.; Moshé, Solomon L. (2005). Models of Seizures and Epilepsy. Burlington: Elsevier. uk. 539. ISBN 978-0-08-045702-4. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 8 Septemba 2017.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. "Gabapentin". International Drug Price Indicator Guide. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 Juni 2018. Iliwekwa mnamo 13 Machi 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  10. Hamilton, Richart (2015). Tarascon Pocket Pharmacopoeia 2015 Deluxe Lab-Coat Edition. Jones & Bartlett Learning. uk. 327. ISBN 978-1-284-05756-0.
  11. "The Top 300 of 2020". ClinCalc. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 12 Februari 2021. Iliwekwa mnamo 11 Aprili 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  12. "Gabapentin - Drug Usage Statistics". ClinCalc. 23 Desemba 2019. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 11 Aprili 2020. Iliwekwa mnamo 11 Aprili 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  13. Henney JE (Agosti 2006). "Safeguarding patient welfare: who's in charge?". Annals of Internal Medicine. 145 (4): 305–7. doi:10.7326/0003-4819-145-4-200608150-00013. PMID 16908923.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)