Gallus Steiger

Gallus Steiger (29 Machi 187926 Novemba 1966) alikuwa mmsionari, abate na askofu wa Peramiho, Songea, Tanzania.

Alizaliwa huko Bueron, Uswisi. Alisoma katika shule maarufu ya Abasia ya Wabenediktini huko Einsiedeln, Uswisi. Mwaka 1902 alifunga nadhiri za utawa kama Mbenediktini huko St.Ottilien (Ujerumani). Alitumwa kama mmisionari na kufika Dar es Salaam 04/06/1906. Baada ya kushinda Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, Waingereza waliwafukuza wamisionari wenzake Wajerumani, lakini yeye kama raia wa Uswisi hakufukuzwa. Mwaka 1920 aliruhusiwa kuendelea na umisionari huko Ndanda kusini mashariki mwa nchi Tanganyika. Mwaka 1922 aliteuliwa kuwa Prefect Apostolic wa huko Lindi na akawa mkuu wa wamisionari Wabenediktini. Mwaka 1928 alikuwa Abate (mwanzoni mwa Lindi na mwaka 1931 Abate wa Peramiho) na alipata wakfu kuwa askofu mwaka 1934 huko Einsiedeln. Alistaafu 1953 na kufa huko Peramiho 1966. Alizikwa kwenye kanisa kuu la Peramiho.

Viungo vya njeEdit