Gegereka
Kaa tunga (Scylla serrata)
Kaa tunga (Scylla serrata)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye mwili wa pingili na miguu ya kuunga wasio na ugwe wa mgongo)
Nusufaila: Crustacea (Gegereka: Arithropodi walio na kiunzi-nje chenye kaboneti ya kalisi)
Brünnich, 1772
Ngazi za chini

Ngeli na nusungeli:

Gegereka ni arithropodi walio na viungo vyenye matagaa mawili na kiunzi-nje ngumu ambacho kimeumbwa kwa khitini na kaboneti ya kalisi. Mifano ni kaa, kamba, kambakoche na uduvi. Takriban spishi zote zinatokea majini, baharini hasa. Spishi kadhaa za kaa na nusuoda moja (Oniscidea au woodlice) zinatokea nchini kavu. Spishi nyingine za gegereka zimegundishwa kwenye tabaka la chini (kombe-bata na vipele-bahari) na nyingine tena ni vidusia (bamvua na minyoo-ulimi).

Kama takriban arithropodi wote kiwiliwili cha gegereka wa kawaida kina sehemu tatu: kichwa au kefalo (cephalon), kidari au toraksi (thorax) na fumbatio au pleo (pleon). Pengine kichwa na kidari vimeunganishwa katika kefalotoraksi (cephalothorax). Idadi ya pingili inatofautiana baina ya familia mbalimbali. Mfano wa idadi ni kama ifuatavyo: 5 katika kichwa, 8 katika kidari na 6 katika fumbatio. Kila pingili inaweza kubeba viungo lakini si lazima. Vile vya kichwa ni jozi mbili za vipapasio, jozi moja ya mandibili na jozi mbili za maksila; vile vya kidari ni jozi tatu za maksilipedi na jozi tano za pereiopodi; na vile vya fumbatio ni jozi tano za pleopodi na jozi moja ya uropodi. Jozi moja hadi tatu za pereiopodi hubeba magondi.

Uainishaji

hariri

Uainisho wa kawaida wa gegereka unaonyeshwa katika sanduku la uainishaji. Lakini tangu mwanzo wa karne hii maainisho mabadala yamependekezwa yaliyotokana na changanuzi za ADN. Kufuatana na pendekezo la hivi karibuni wadudu wa kweli wamebadilika kutoka kundi la kale la gegereka (tazama pendekezo hili katika ukurasa wa arithropodi).