George Lilanga

'

George Lilanga
Lilanga-Work021-1998.jpg
Amezaliwa1934
Amefariki27 Juni 2005
NchiTanzania
Kazi yakeMchongaji vinyago
Mchoraji


George Lilanga (1934 - 27 Juni 2005) alikuwa msanii Mmakonde kutoka Tanzania.

Alipokuwa bado kijana alijifunza kuchonga sanamu jinsi ya Kimakonde. Lakini baadaye alianza kuchora pia akitumia hasa rangi za mafuta. Aliishi Dar es Salaam. Mwaka wa 1974 aligunduliwa kuwa na kisukari. Ndio ugonjwa uliosababisha kifo chake.

Kazi yake ilioneshwa katika Afrika Remix huko Dusseldorf, Paris, London na Tokyo

WasifuEdit

Mahali na siku aliyozaliwa havijulikani, lakini labda alizaliwa mwaka 1934. Alizaliwa bila shaka kijiji cha Kikwetu katika wilaya ya Masasi, huko Tanzania Kusini. Wazazi wake walikuwa wamakonde na kabila la wamakonde linatoka Msumbiji. Baba yake alikuwa mkulima. Baadaye, baba yake aliondoka na familia yao na alioa mwanamke mwingine. 

Wakati Lilanga alipokuwa mtoto, yeye na familia yake walisogea Dar es Salaam. Baada ya sekondari, alianza kufanya sanaa ya uchongaji. Alianza uchongaji kwa kutumia mbao laini, mizizi, na mbao za mti wa ebony pamoja na kuonesha desturi ya wamakonde kwenye kazi zake. Alitumia maarifa kutoka mwaka 1961 hadi mwaka 1972. Katika Msumbiji, watu wa Ulaya wanaipenda sana sanaa yake. Katika mwaka wa 1970, Lilanga alienda tena Dar es Salaam kwa sababu alidhani ni bora zaidi kuuza sanaa jijini.

Taaluma yake ya usaniiEdit

Katika mwaka wa 1971, Lilanga alipata kazi yake ya kwanza katika Nyumba ya Sanaa. Alikuwa mchongaji wa usiku, lakini wasanii wengine waliona sanaa na uchongaji wa Lilanga na walimwambia Lilanga ajiunge na Nyumba ya Sanaa. Katika mwaka wa 1972, alianza kupaka rangi na katika mwaka wa 1974, alikuwa na sanaa katika Makumbusho ya Taifa ya Dar es Salaam. 

Katika mwaka wa 1974, Alichoka sana na hakuweza kuendelea kuchonga vinyago pekeyake. Lilanga alienda kumuona daktari kutokana na uchovu wa mara kwa mara na aligundulika kuwa na maradhi ya kisukari. 

 
George Lilanga akiwa na sanaa yake We Banana Anangalia Ulimi Kiangu Unawasha.

Katika mwaka wa 1977, alienda New York na aliuza sanaa zake katika jiji la Manhattan. Yeye alikuwa mshirikiri kwenye maonesho pia. Baadaye, katika Washington D.C. alishiriki pamoja na wasanii wa nchi mbalimbali za Afrika kwenye enesho kubwa la sanaa. Alikuwa na bahati katika Marekani, Ulaya, Afrika, India, na Japani pia. 

Katika miaka ya 1980, sanaa yake ilikuwa kubwa sana pengine mita moja ya mraba. Kwa kawaida, alitumia rangi ya mafuta kupaka kazi zake za sanaa. Katika miaka ya 1990, alikuwa na mapumziko ya muda mrefu kwasababu ya ugonjwa wa kisukari, ni gonjwa mbaya sana. Alisitisha kazi yake kwa sababu ilikuwa vigumu sana. Alianza kufundisha wanafunzi wengine kuchora na kupaka rangi.

Katika mwaka wa 2000, afya yake ilikuwa mbaya sana kwa sababu alikuwa na kisukari, shinikizo la damu, na magonjwa ya moyo. Alitumia kiti cha ulemavu kutembelea, lakini alifanya sanaa. Halafu mwaka wa 2001, hakuweza kufanya sana. Sanaa ilikuwa kwa nadra na kwa vitu rahisi kuchora. 

Lilanga alifariki Jumatatu ya tarehe 27, mwezi wa sita, mwaka wa 2005, mjini Dar es Salaam.  Kuna sanaa ya Lilanga katika The Contemporary African Art Collection (CAAC) na Hamburg Mawingu Collection huko Ujerumani pia. Sanaa hiyo ni nzuri sana na ina rangi za kuvutia sana. George Lilanga alikuwa msanii muhimu sana wa Afrika Mashariki na sanaa zake za Kimakonde zilifanikiwa.

  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu George Lilanga kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.