Ghuba ya Akaba
Ghuba ya Akaba (Kar. Bahr al-'Aqaba; pia: Ghuba ya Eilat) ni mkono wa kaskazini-mashariki ya Bahari ya Shamu. Imetenganisha Bara Arabu na Rasi ya Sinai. Kijiolojia ghuba ni sehemu ya Bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki.
Nchi zinazopakana na ghuba hii ni hasa Misri na Uarabuni wa Saudia. Yordani na Israeli zina pwani fupi kwenye ncha ya kaskazini kabisa ya ghuba.
Bandari muhimu ni Akaba upande wa Yordani na Eilat upande wa Israeli pamoja na Taba wa Misri.
Ghuba inanaza kwenye mlango wa bahari wa Tiran. Urefu kutoka hapa hadi Akaba ni kilomita 175. Upana wa ghuba ni takriban 25 - 30 km. Kina kikubwa ni 127 m.
Ghuba hupendwa na watalii wanaopumzika na kuangalia samaki chini ya maji. Mazingira yake ni hasa jangwa.