Ghuba ya Omani
(Elekezwa kutoka Ghuba ya Oman)
Ghuba ya Omani (Kar.: خليج عمان khalij 'uman; Kiajemi: دریای عمان daryaye oman) ni mkono wa kaskazini-magharibi wa Bahari Hindi unaofikia hadi mlango wa Hormuz unapoendelea katika Ghuba ya Uajemi.
Urefu wake ni 560 km. Upande wa magharibi maji yana kina cha m 50 na upande wa mashariki kina cha mita 200.
Ghuba ya Uajemi ni muhimu sana kiuchumi, kisiasa na kijeshi kwa sababu ni mlango wa kuingia na kutoka Ghuba ya Uajemi penye asili ya sehmu kubwa ya mafuta ya petroli duniani.
Ghuba imepakana na Uajemi, Falme za Kiarabu na Omani.