Gogo (wingi: magogo) ni shina la mti lililokatwa. Mara nyingi huwa na maumbo ya mviringo na linatokana na miti mikubwa.

Magogo msituni.

Magogo hutumika kwa kazi mbalimbali, kama vile kuni za kupikia, kutengeneza nguzo za ujenzi wa nyumba za jadi, au kutengeneza samani na vyombo vya nyumbani. Aidha, gogo linaweza kutumiwa kama nyenzo ya kuchonga sanamu na kazi za mikono.


Makala hii kuhusu "Gogo" ni fupi mno. Inahitaji kupanuliwa mapema.