Grace Gao (mwanaharakati)

Grace Gao (anajulikana pia kama Grace Geng[1]; amezaliwa 1993) ni mwanaharakati wa haki za binadamu nchini Uchina. Yeye ni binti Gao Zhisheng, wakili wa Kichina wa haki za binadamu na mpinga sera za serikali.[2][3] Yeye na familia yake wamepelelezwa, kupigwa, na kutishwa na mamlaka za Uchina.[3] Anaelimisha kimataifa ili kutangaza kitabu cha baba yake A China More Just na kutilia mkazo kwenye kesi yake (kwa sasa, ametoweka na mamlaka za Uchina zinahusika na kutoweka kwake[4]), na kusema dhidi ya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Uchina.[3] "Kwa hiyo, ninajikuta katika nafasi ya kuchukua vazi hilo na kuwa mtetezi wa haki za binadamu kama baba yangu... Ukweli ni nguvu na nitaendelea kuongea mpaka baba yangu awe huru".[5][6]


Maisha ya awali hariri

Gao alikuwa akisindikizwa kwenda shuleni kila siku na maafisa wa polisi ambao walimfuata kila alikoenda.[3] Grace alijijeruhiwa kwa sababu ya huzuni na maumivu[7] na, akiwa na umri wa miaka 17, alijaribu kujiua mara kadhaa.[2] Alipata ugumu kuelewa maamuzi ya baba yake.[2]

Baada ya Gao kuzuiwa na serikali kuhudhuria shule,[3] mama yake aliamua kuwasafirisha yeye pamoja na kaka yake (Peter, b. 2005) kutoka Uchina.[3] Mnamo tarehe 9 Januari 2009, walikimbilia Uthai kwa usafiri wa pikipiki na basi (wakiwa wamejificha kwenye sehemu ya kubeba mizigo),[8] kisha wakaenda Merika ambako walipewa hifadhi ya kisiasa.[8][9] Huko New York, Grace alipata matibabu hospitalini kwa miezi sita kwa maswala ya afya ya akili lakini bado ilikua ngumu kuamini watu.[2] Alijifunza kumwelewa baba yake[8] na kumsaidia.[2]

Elimu hariri

Grace alijifunza Kiingereza baada ya kuhamia Merika, alihitimu shule ya upili akiwa na miaka 20,[8] na kuendelea kusoma uchumi katika chuo kikuu cha California.[2]

Marejeo hariri

  1. "Grace Geng: Chinese dissident's daughter proud of her 'brave' father", BBC News (in en-GB), 2016-06-14, retrieved 2021-09-16 
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 2.5 "Citizen Power Initiatives for China", Wikipedia (in English), 2021-01-05, retrieved 2021-09-16 
  3. 3.0 3.1 3.2 3.3 3.4 3.5 Grace Gao | Speakers | Oslo Freedom Forum. web.archive.org (2017-08-15). Jalada kutoka ya awali juu ya 2017-08-15. Iliwekwa mnamo 2021-09-16.
  4. A year on, lawyer's disappearance highlights China's escalating human rights disaster (en-GB). Hong Kong Free Press HKFP (2018-08-13). Iliwekwa mnamo 2021-09-16.
  5. Av Hanne Mauno. – Jeg var sjokkert. Men jeg har vokst opp i et Kina som hjernevasket meg. (no). Dagsavisen. Iliwekwa mnamo 2021-09-16.
  6. Grace Geng, 'Truth is power and I will keep speaking it until my father is free'(03/10/16) for International Service for Human Rights Archived 25 Juni 2021 at the Wayback Machine. Iliwekwa mnamo 2021-09-16
  7. 'My Father Never Spoke About The Persecution He Suffered' (en). Radio Free Asia. Iliwekwa mnamo 2021-09-16.
  8. 8.0 8.1 8.2 8.3 A Hero’s Daughter (en-US). National Review (2017-06-25). Iliwekwa mnamo 2021-09-16.
  9. hermesauto (2016-06-14). China rights lawyer Gao Zhisheng ready for consequences over new book: Daughter (en). The Straits Times. Iliwekwa mnamo 2021-09-16.