Guinness Nigeria ni sehemu ya kampuni kubwa inayojulikana iitwayo Diageo plc iliyoko Uingereza, iliingizwa mwaka 1962 kwa ujenzi wa kituo cha pombe huko Ikeja, moyo wa Lagos. Kituo hiki kilikuwa cha kwanza nje ya Ireland na Uingereza. Vituo vingine vilifunguliwa baadaye kama kituo cha Bennin, mwaka 1974, na cha Ogba, mwaka 1982.

Foreign Extra Stout, bidhaa kuu ya Guinness Nigeria. Angalia pia chapa ya nyuma

Guinness Nigeria inajulikana kwa chapa maarufu za hali ya juu zikiwemo, Foreign Extra Stout(1962), Guinness Extra Smooth(2005), Malta Guinness(1990), Harp Lager Beer(1974), Gordon's Spark(2001), Smirnoff Ice(2006) na Satzenbrau(2006).

Kampuni ya Guinness Nigeria plc ni kampuni ambayo inaamini katika kuendeleza jamii yake. Imeweza kufanya hivi kwa kujiingiza katika miradi mizuri ya jamii kadhaa nchini Nigeria. Miradi hii ni kama; Water of Life Initiative, ambayo inatoa maji ya bomba kwa wanigeria kama 500,000 waliotawanyika katika maeneo ya mashambani, udhamini kwa wanafunzi, mahospitali ya macho ya Guinness katika miji mitatu nchini Nigeria.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Guinness Nigeria kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.