Guselkumab, inayouzwa kwa jina la chapa Tremfya, ni dawa inayotumika kutibu ugonjwa wa ngozi kavu iliyoinuka yenye kuwasha na iliyo na mabaka (plaque psoriasis).[1][2] Dawa hii inatumika kwa ugonjwa wa wastani hadi mkali.[1] Inatolewa kwa sindano chini ya ngozi.[1]

Guselkumab ?
Monoclonal antibody
Aina Whole antibody
Chanzo Binadamu
Lengo IL23
Data ya kikliniki
Majina ya kibiashara Tremfya
AHFS/Drugs.com Monograph
MedlinePlus a617036
Taarifa za leseni US Daily Med:link
Kategoria ya ujauzito B1(AU)
Hali ya kisheria Prescription Only (S4) (AU) POM (UK) -only (US)
Njia mbalimbali za matumizi Chini ya ngozi
Vitambulisho
Nambari ya ATC ?
Data ya kikemikali
Fomyula C6402H9864N1676O1994S42 

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na maambukizi ya sehemy ya juu ya njia ya upumuaji.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha maambukizi, maumivu ya kichwa, maumivu ya viungo, matatizo ya ini na kupungua kwa ufanisi wa chanjo.[3] Usalama wa matumizi yake katika ujauzito hauko wazi.[3] Dawa hii ni kingamwili ya monokloni ambayo inashikamana na kuzuia interleukin-23.[1]

Guselkumab iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani na Ulaya mwaka wa 2017.[3][1] Nchini Uingereza, iligharimu Huduma ya Afya ya Kitaifa (NHS) takriban £2,250 kwa miligramu 100 kufikia mwaka wa 2021.[4] Kiasi hiki nchini Marekani ni takriban dola 11,600 za Marekani.[5]

Marejeo

hariri
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 "Tremfya". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 22 Novemba 2021. Iliwekwa mnamo 9 Desemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Guselkumab". LiverTox: Clinical and Research Information on Drug-Induced Liver Injury [Internet]. National Institute of Diabetes and Digestive and Kidney Diseases. Juni 2018. PMID 31643594.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. 3.0 3.1 3.2 "Guselkumab Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 27 Septemba 2021. Iliwekwa mnamo 9 Desemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. BNF 81: March-September 2021. BMJ Group and the Pharmaceutical Press. 2021. uk. 1302. ISBN 978-0857114105.
  5. "Guselkumab Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Iliwekwa mnamo 9 Desemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)