Hadj Bouchiba

mwimbaji wa Algeria

Hadj Bouchiba (1903Januari 5, 1957)[1] alikuwa mwandishi wa nyimbo, mtunzi, mshairi na mchoraji.

Picha Ya Hadj Bouchiba
Picha Ya Hadj Bouchiba

Wasifu hariri

Abdelghani Bouchiba alizaliwa Constantine, Algeria mwaka 1903 ila alihamia Algiers akiwa katika umri mdogo pamoja na baba yake Salah aliyekuwa na maduka mawili ya viatu zenye staili za kiarabu huko Casbah. Mwaka 1923 aliishi na wazazi wake Rampe Valée. Aliitwa kuhudumu katika jeshi kisha kupata kazi yake ya kwanza kama fundi na kisha kuwa dereva wa mashine. Baada ya kumaliza kuhudumu jeshi, Bouchiba alijikita zaidi katika muziki kuanzia mwaka 1924 mpaka 1925. Baada ya mwonekano wa mwanzo katika medh chaabi taratibu Bouchiba alichagua El Arrobi ambayo ingepelekea kumpeleka katika ngazi ya juu na iliwavutia watu wa Fahs ambapo Bouchiba alipopata mahali pa kudumu. Januari 5, 1957 Bouchiba alipigwa risasi na La Main Rouge, shirika la siri la kikoloni. Alizikwa katika makaburi ya El Kettar.

Nyimbo hariri

  • Mahl El Djoudi
  • Ya akhina[2]
  • .Ya Doukar Edjnani
  • Sbouhi

Marejeo hariri

  1. "Culture : AYANT EU DE NOMBREUX ADEPTES Le chaâbi entre histoire et théorie". Le Soir d'Algérie. March 9, 2006. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo April 7, 2014. Iliwekwa mnamo April 2, 2014.  Unknown parameter |url-status= ignored (help); Check date values in: |date=, |archivedate=, |accessdate= (help)
  2. performed by Kamel Bourdib