Haki ya Kupata Huduma za Kiafya
Haki za binadamu zilizoelezwa katika Tamko la Haki za Binadamu la Ulimwengu na nyaraka nyingine nyingi
Haki ya Kupata Huduma za Kiafya ni haki inayochagiza kupatikana kwa haki nyingine kama vile haki za kiuchumi, za kijamii na za kiutamaduni ambazo kimsingi kila binadamu anapaswa kupata kwa mujibu wa viwango vya chini vya kimataifa.
Dhana ya haki ya afya imeorodheshwa katika mikataba ya kimataifa ambayo ni pamoja na Tamko la Kimataifa la Haki za Binadamu, Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiuchumi, Kijamii na Kiutamaduni, na Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu.
Kuna mijadala juu ya tafsiri na matumizi ya haki ya afya kwa kuzingatia namna haki ya kupata huduma za kiafya inavyofafanuliwa, ni haki gani zinazojumuishwa katika haki hiyo, na ni taasisi zipi zina jukumu la kuhakikisha haki hiyo inapatikana. [1]
Marejeo
hariri- ↑ "Human Rights Measurement Initiative – The first global initiative to track the human rights performance of countries". humanrightsmeasurement.org. Iliwekwa mnamo 2022-03-09.
Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Haki ya Kupata Huduma za Kiafya kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |