Halima James Mdee

(Redirected from Halima Mdee)

Halima James Mdee (alizaliwa Makanya, Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro, 18 Machi 1978) ni mbunge wa viti maalum katika bunge la Tanzania kupitia chama pinzani cha CHADEMA.

MaishaEdit

Halima James Mdee ni mtoto wa mwisho katika familia ya Profesa James Mdee ambaye alikuwa mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mdee alizaliwa katika familia ya Wakristo na alibatizwa na kuitwa Theodosia, hata hivyo anatumia zaidi jina alilorithi kutoka kwa bibi yake mzaa baba, Halima. Ukoo wake ni waumini wa dini ya Kiislamu, isipokuwa baba yake na kaka yake ambao walibatizwa na familia yao ikaridhia wawe Wakatoliki. Kikabila ni Mpare.

ElimuEdit

Alianza kusoma elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Mlimani jijini Dar es Salaam mwaka 1985 na kuhitimu mwaka 1991. Alichaguliwa kujiunga na Shule ya Sekondari ya Wasichana Zanaki mwaka 1992 na kuhitimu kidato cha nne mwaka 1995.

Mwaka 1996 hadi 1998 alisoma kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Kilakala mkoani Morogoro na 1999 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako alisomea sheria na kuhitimu mwaka 2003. Aliendelea kusoma shahada ya uzamili ya sheria katika chuo kikuu cha Pretoria (Afrika Kusini) [1] mwaka 2006 hadi 2007. [2]

Kazi na SiasaEdit

Alipata ajira katika Wizara ya Kazi na Maendeleo ya Vijana mwaka 2004 akiwa Ofisa Maendeleo kama mwanasheria mpaka mwaka 2005 alipoamua kuacha kazi na kuingia katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, ambako alishiriki kuwapigia kampeni wagombea mbalimbali wa CHADEMA kabla ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa viti maalumu.

Vyeo vya ChamaEdit

Mbali na ubunge, pia ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Taifa la CHADEMA, Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la CHADEMA na ofisa katika kurugenzi ya sheria.

TanbihiEdit

Viungo vya njeEdit

  Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Halima James Mdee kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.