Halotel
Kampuni ya Viettel Tanzania Public Limited inayojulikana kibiashara kama Halotel, ni kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi inayotoa huduma za sauti, ujumbe, data, na mawasiliano nchini Tanzania. Inamilikiwa na Viettel Global JSC, ambayo ni kampuni ya uwekezaji ya serikali ya Vietnam inayowekeza katika sekta ya mawasiliano duniani kote[1].
Halotel imewekeza zaidi ya Dola za Kimarekani bilioni 1 katika soko la mawasiliano la Tanzania. Kampuni hii ilikuwa ya kwanza nchini kuruhusiwa kuweka kebo ya fiber optic na imeweka zaidi ya kilomita 18,000 za nyaya hizo, kuhakikisha huduma za mawasiliano zinapatikana katika mikoa yote 26 ya Tanzania.
Tanbihi
hariri- ↑ "Viettel to launch in Tanzania in Oct-15 under Halotel banner". TeleGeography. Primerica. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-04. Iliwekwa mnamo 2015-12-20.
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Halotel kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |