Haru Mutasa ni mtangazaji wa Al Jazeera ya Kiingereza, afisi ya Nairobi. Al Jazeera ya Kiingereza ni stesheni ya kwanza inayotoa habari kwa lugha ya Kiingereza iliyo na makao yake makuu katika nchi ya Kiarabu.[1][2]

Yeye amewahi kufanya kazi na South African Broadcasting Corporation (SABC), CNN, Television New Zealand (TVNZ), Associated Press Television News (APTN) na Star Sports Network.

Kama ripota mjini Harare, Zimbabwe, Haru aliwahi kuripoti taarifa nyingi kuhusu Zimbabwe zilizoonyeshwa katika kipindi cha Inside Africa (CNN), Television New Zealand (TVNZ) na APTN.

Mwaka wa 2007, Haru aliteuliwa kwa "Young Journalist of the Year" (Mwanahabari Mdogo Zaidi katika Mwaka huo) katika tuzo ya Royal Television Society.

Marejeo

hariri

Viungo vya nje

hariri