Hataza (Kiingereza patent) ni haki ya kisheria anayopewa mbunifu ya kukataza mtu mwingine asichukue au kuiga ubunifu wake bila idhini yake. Mtoa haki ni serikali ya nchi kufuatana na sheria husika.

Hataza inaunda haki ya mwenye hataza kuzuia wengine wasitengeneze, wasitumie au wasiuze ubunifu wake kwa muda wa miaka fulani baada ya kuandikishwa kwa uvumbuzi katika ofisi ya hataza ya serikali[1]. Haki ya hataza inakuja pamoja na wajibu wa kueleza hadharani muundo na upekee wa ubunifu.

Nchini muda wa hataza ni tofauti kati ya nchi na nchi. Tanzania kuna kipindi cha miaka 20 kuanzia kukabidhi kwa hati ya hataza kwa wakala wa serikali.[2] .

Marejeo

hariri
  1. Nchini Tanzania utoaji wa hataza uko chini ya Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (Business Registrations and Licensing Agency BRELA) https://www.brela.go.tz/index.php/companies/ors_info Ilihifadhiwa 1 Desemba 2021 kwenye Wayback Machine.
  2. Patents Ilihifadhiwa 6 Mei 2022 kwenye Wayback Machine. , tovuti ya BRELA, Tanzania