Havilland de Sausmarez

Havilland de Sausmarez (1861 - 1941)[1] alikuwa hakimu wa mahakama kadhaa za Uingereza za kikoloni huko Afrika na Asia, Dola la Osmani na China.

Nafasi yake ya mwisho ya mahakama kabla ya kustaafu ilikuwa kama Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Uingereza kwa China.

Maisha ya awali hariri

Sausmarez alizaliwa mnamo tarehe 30 Mei 1861, ni mtoto wa Mchungaji.

Havilland de Sausmarez alifunga ndoa na Anne Priaulx Walters. Alikuwa mwanafunzi huko Westminster, ambapo alikuwa na rekodi mwanariadha bora, pamoja na kuwa mwogeleaji bora.

Baada ya hapo alikwenda Chuo cha Trinity, Cambridge, ambapo alihitimu BA mnamo mwaka 1883. Mnamo mwaka 1881, alipokuwa huko Cambridge.

Uteuzi wa kimahakama hariri

 
Mchoro wa Havilland De Sausmarez

De Sausmarez alijiunga na huduma ya Mahakama ya Mambo ya nje wakati alipoteuliwa kuwa Balozi wa Zanzibar mnamo mwezi Juni mwaka 1892.

Alishikilia ofisi ya Jaji Msaidizi wa Mahakama ya ubalozi huko Zanzibar kuanzia mwaka 1893-1897 na kisha akashika ofisi ya Jaji Msaidizi wa Mahakama Kuu ya Kibalozi kwa Dola ya Ottoman.

Aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Dola ya Ottoman mnamo mwaka 1903 hadi mwaka 1905.

Mnamo mwaka 1905, de Sausmarez aliteuliwa kuwa Jaji wa mahakama Kuu ya Uingereza kwa China na Korea (iliyoko mjini Shanghai). Alitumikia wadhifa huo hadi mwaka 1921. Kwa nguvu ya nafasi yake kama jaji wa Mahakama Kuu huko Shanghai alikuwa kama Rais wa Mahakama Kuu ya Hong Kong kuanzia mwaka 1910 hadi mwaka 1920.

Kurudi Guernsey hariri

Sausmarez alistaafu mnamo mwaka 1920.[2] Baada ya kuondoka Shanghai, Sausmarez aliweka makazi yake katika Sausmarez Manor huko Guernsey. Mke wake, Annie, Lady de Sausmarez, GBE, alikuwa mhisani.

Tanbihi hariri

  1. Fisher, Hugh A. (1898). The Cathedral Church Of Hereford : a description of its fabric and a brief history of the episcopal see. London: George Bell & Sons. ISBN 600-00-0000-6. OCLC 670484843. 
  2. Volume 1920 - Issue 2735 (1920-01-10). The North China Herald Online. Iliwekwa mnamo 2020-02-23.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Havilland de Sausmarez kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.