Bawasiri
Bawasiri (au Kikundu au Futuri au Puru au Mjiko au Hemoroidi kutoka Kiingereza hemorrhoid) ni hali ya kutuna kwa mishipa ya damu katika mfereji wa njia ya haja kubwa ambayo husaidia kudhibiti kinyesi.[1][2] Katika hali yake ya fiziolojia, hutenda kazi kama mto uliotengenezwa kwa njia ya vena na tishu unganishi. Huwa patholojia ikiwa hufungana [3] kwa kuvimba au kupata inflamesheni.
Hemorrhoids | |
---|---|
Mwainisho na taarifa za nje | |
Kundi Maalumu | General surgery |
ICD-10 | I84. |
ICD-9 | 455 |
DiseasesDB | 10036 |
MedlinePlus | 000292 |
eMedicine | med/2821 emerg/242 |
MeSH | D006484 |
Dalili za hemoroidi hulingana na mahali. Hemoroidi za ndani kwa kawaida hujitokeza kwa kinyesi kilicho na damu bila maumivu, ilhali hemoroidi za nje zinaweza kutoa dalili chache au ikiwa zina thrombasi maumivu na uvimbe katika sehemu ya njia ya haja kubwa. Watu wengi hurejelea kimakosa dalili yoyote inayotokea karibu na sehemu ya rektamu ya njia ya haja kubwa kuwa "hemoroidi" na visababishi hatari vya dalili vinapaswa kutupiliwa mbali. Huku kisababishi halisi kikisalia kutojulikana, baadhi ya vipengele vinavyoongeza shinikizo la fumbatio la ndani, hasa kufungika kwa choo, vinaaminika kuchangia ukuaji wa hemoroidi.
Matibabu ya mwanzo ya maradhi madogo hadi yale ya kawaida huwa na ongezeko la kula chakula kilicho na faiba, vinywaji ili kudumisha haidresheni, dawa za kutibu inflamesheni husaidia kwa maumivu, na mapumziko. Baadhi ya taratibu ndogo zinaweza kutekelezwa ikiwa dalili ni kali au hazistawi kwa mwelekeo wa kudhibiti usiobadilika. Upasuaji hutengewa wanaokosa kuonyesha mabadiliko. Hadi nusu ya idadi ya watu wanaweza kuwa na matatizo na hemoroidi kwa wakati fulani maishani mwao. Matokeo kwa kawaida huwa mema.
Dalili na ishara
haririHemoroidi za ndani na za nje zinaweza kujitokeza vitofauti; hata hivyo, watu wengi wanaweza kuwa na zote mbili.[2] Kuvuja damu kunakotosha kusababisha anemia ni nadra,[4] na uvujaji wa damu unaohatarisha maisha ni nadra.[5] Watu wengi wanaweza kuona haya wanapokumbana na tatizo[4] na mara nyingi hutafuta matibabu tu wakati hali inapozidi.[2]
Za nje
haririIkiwa hazina thrombasi, hemoroidi za nje zinaweza kusababisha matatizo machache.[6] Hata hivyo, zinapokuwa na thrombasi, zinaweza kuwa na maumivu sana.[2][3] Hata hivyo, maumivu haya huisha kwa muda wa siku 2 - 3 .[4] Hata hivyo uvimbe unaweza kuchukua wiki chache kupotea.[4] kishikizo cha ngozi kinaweza kubaki baada ya kupona.[2] Ikiwa hemoroidi ni kubwa na zinasababisha madhara, zinaweza kusababisha mwasho wa ngozi iliyo karibu na pia kwa njia ya haja kubwa.[6]
Za ndani
haririHemoroidi za ndani kwa kawaida hujitokeza kwa uwekundu uliyo ng’aavu, bila maumivu kuvuja damu kwa rektamu wakati wa au kufuatia kusonga kwa utumbo.[2] Damu hufunika kinyesi, hali inayoitwa kinyesi kilicho na damu, huwa kwa karatasi ya chooni, au hudodoka katika bakuli ya choo.[2] Kinyesi chenyewe kwa kawaida huwa chenye rangi.[2] Dalili zingine zinaweza kuwa ni pamoja na kutoka kwa ute, kuzungukia njia ya haja kubwa ikiwa utashuka kupitia njia ya haja kubwa, mwasho, na kutoweza kuzuia kinyesi.[7][5] Hemoroidi za ndani kwa kawaida huwa na maumivu tu ikiwa zitakuwa na thrombasi au nekrotiki.[2]
Visababishi
haririKisababishi kamili cha hemoroidi hakijulikani.[8] Baadhi ya vipengele vichangiapo ni pamoja na: Mazoea ya utumbo yasiyojirudia (kufungika kwa choo au kuhara), ukosefu wa mazoezi, visababishi vya lishe (chakula kilicho na kiwango cha chini cha faiba), ongezeko la shinikizo la ndani la fumbatio (uchovu unaoendelea kwa muda, asitisi, ukubwa wa ndani wa fumbatio, au ujauzito), jenetiki, kutokuwepo kwa vali katika vena ya hemoroidi, na kuongezeka kwa umri.[3][4] Visababishi vingine vinayoaminiwa kuongeza hatari ni pamoja na unene, kuketi chini kwa muda mrefu,[2] kikohozi kinachoendelea kwa muda na sakafu ya pelvisi kutofanya kazi.[9] Hata hivyo, thibitisho la miungano hii, ni ya chini.
Wakati wa ujauzito, shinikizo kutoka mimba kwa fumbatio na ubadilishaji wa homoni hufanya mishipa ya hemoroidi kuwa kubwa. Kuzaa pia husabibisha ongezeko la shinikizo la ndani la fumbatio.[10] Ni nadra kwa wanawake wajawazito kuhitaji matibabu ya upasuaji, kwa sababu dalili huisha baada ya kuzaa.[3]
Pathofisiolojia
haririMito ya hemoroidi ni sehemu ya anatomi ya kawaida ya binadamu na huwa maradhi inapopitia mabadiliko yasiyo ya kawaida.[2] Kunayo mito tatu iliyo katika mfereji wa njia ya haja kubwa wa kawaida.[3] Hii huwa pembeni mwa kushoto, utangulizi wa kulia, na sehemu za nyuma za kulia.[4] Zimetengenezwa kwa mishipa ya damu inayoitwa sinasi, tishu unganishi na misuli nyororo bali si kwa ateri wala vena.[9] Sinasi haziwi na tishu za misuli katika kuta zao zinazotofautisha kutoka kwa vena zake.[2] Seti hii ya mishipa ya damu huitwa pleksasi ya hemoroidi.
Mito ya hemoroidi ni muhimu kwa kushikilia. Huchangia hadi asilimia 15–20% ya shinikizo la kufungika kwa njia ya haja kubwa wakati wa kupumzika na kukinga misuli ya spinkta ya njia ya haja kubwa wakati wa kupitisha kinyesi.[2] Mtu anapoketi chini, shinikizo la ndani la fumbatio huongezeka, na mito ya hemoroidi kuongezeka kwa ukubwa ikisaidia kudumisha kufungika kwa njia ya haja kubwa.[4] Inaaminika kuwa dalili za hemoroidi hutokea wakati miundo hii ya mishipa huteleza upande wa chini au wakati shinikizo la vena linaongezeka sana.[5] Ongezeko la spinkta ya njia ya haja kubwa shinikizo pia linaweza kuhusishwa katika dalili za hemoroidi.[4] Aina mbili za hemoroidi hutokea: Za ndani kutoka kwa pleksasi kubwa ya hemoroidi na za nje kutoka kwa pleksasi ndogo ya hemoroidi.[4] mstari wa denteti Hugawanya sehemu zote mbili ya hemoroidi.[4]
Utambuzi
haririGrade | Diagram | Picture |
---|---|---|
1 | ||
2 | ||
3 | ||
4 |
Hemoroidi hutambuliwa kwa uchunguzi wa kimwili.[11] Uchunguzi wa kutazama njia ya haja kubwa na maeneo yaliyo karibu na njia ya haja kubwa yanaweza kutambua hemoroidi za nje au zile zilizoshuka.[2] uchunguzi wa rektamu unaweza kufanywa ili kutambua uwezekano wa tyuma, ya rektamu polipsisi, prosteti iliyo kubwa, au jipu.[2] Uchunguzi huu unaweza kutofaulu bila utulizaji unaofaa kwa sababu ya maumivu ,Hata ingawa hemoroidi nyingi hazihusiani na maumivu.[3] Udhibitishaji wa kutazama kwa hemoroidi za ndani unaweza kuhitaji anoskopu, kifaa cha bomba tupu kilicho na mwanga ulioshikishwa katika mwisho wa upande mmoja .[4] Kunazo aina mbili za hemoroidi: Za nje na za ndani. Hizi zinatofautishwa na mahali zilipo kwa kuzingatia mstari wa denteti .[3] Watu wengine wanaweza kuwa na aina zote mbili za dalili kwa wakati mmoja.[4] Ikiwa maumivu yapo kuna uwezekano mkuu wa hali kuwa kupasuka kwa njia ya haja kubwa au hemoroidi ya nje kuliko ile ya ndani.[4]
Za ndani
haririHemoroidi za ndani ni zile ambazo huanza kutokea juu ya mstari wa denteti.[6] Huwa zimefunikwa na kolamu ya epitheliumu ambayo haina maumivu risepta inayopitisha hisia. Ziliainishwa mwaka wa 1985 katika viwango vinne kwa kuzingatia kiwango cha prolapsi.[3]
- Kiwango I: Hakuna prolapsi. Mishipa tu ya damu inayoonekana.[11]
- Kiwango II: Kuna prolapsi mtu anapoketi lakini inapungua yenyewe.
- Kiwango III: Kuna prolapsi mtu anapoketi na huhitaji kupunguzwa kwa mkono.
- Kiwango IV: Kuna prolapsi na haiwezi kupunguzwa kwa mkono.
Za nje
haririHemoroidi za nje Ni zile zinazotokea chini ya denteti au mstari wa pektineti.[6] Zimefunikwa kwa karibu na anodemu na kwa umbali na ngozi, zote huwa na hisia za maumivu na halijoto.
Utofautisho
haririShida nyingi za njia ya haja kubwa, zikiwa pamoja na kufa kwa mkundu, kupasuka kwa mkundu, jipu, saratani ya kolorekto, varisesi ya mkundu na mwasho wa mkundu huwa na dalili sawa na zinaweza kutambuliwa kimakosa kama hemoroidi.[3] Kuvuja damu kwa rektamu kunaweza pia kusababishwa na saratani ya kolorektamu, kolitisi ikiwa ni pamoja na maradhi ya inflamesheni ya utumbo, maradhi ya divetikula, na anjeodisplasia.[11] ikiwa kuna anemia, uwezekano wa visababishi vingine unapaswa kuchunguzwa.[4]
Hali nyingine zinazosababisha vidonge vya mkunduni ni pamoja na: kishikizo cha ngozi, kuchunjuka kwa mkundu, prolapsi ya rektamu, polipsi na pupila ya mkundu iliyo kubwa.[4] varisesi ya rektamu ya mkundu kwa sababu ya ongezeko la pota hipatensheni (shinikizo la damu katika mfumo wa pota ya vena) unaweza kujitokeza sawa na hemoroidi lakini ni hali tofauti.[4]
Kinga
haririBaadhi ya vigezo vya kukinga vimependekezwa vikiwa ni pamoja na kutojikaza unapoenda haja kubwa, kuepukana na choo iliyofungika au kuhara kwa kula chakula kilicho na kiwango cha juu cha faiba na kunywa vinywaji vingi au kula nyongeza ya faiba, na kupata mazoezi ya yanayotosha.[12][4] Kutumia muda mchache ukienda haja kubwa, kutosoma ukiwa chooni ,[3] na pia kupunguza uzito kwa wale ambao wana uzito ulio mwingi zaidi na kuepukana na uinuaji wa vitu vizito.[13]
Udhibiti
haririUtunzaji
haririMatibabu ya kutunza huwa na lishe iliyo na faiba ya chakula, unywaji wa vinywaji ili kudumisha hidrasheni, madawa ya kuzuia inflamesheni yasiyo na steroidi (Dawa za kutibu inflamesheni), uogaji katika hali ya kuketi, na kupumzika.[3] Ongezeko la ulaji wa faiba umeonyeshwa kuboresha matokeo,[14] na hili linaweza kufanyika kwa kubadilisha chakula au kwa kula nyongeza ya faiba.[3][14] Dhibitisho la faida kutokana na uogaji katika hali ya kukaa katika wakati wowote wa matibabu hata hivyo unakosekana.[15] Ikiwa zitatumika zinapaswa kupimiwa kuwa hadi dakika 15 kwa kila wakatiI.[9]
Wakati ajenti nyingi na sapozitorisi zinapatikana kwa matibabu ya hemoroidi, kunalo dhibitisho ndogo la kudhibitisha matumizi yake.[3] Steroidi zilizo na ajenti hazipaswi kutumiwa kwa muda wa zaidi ya siku 14 zinaweza kusababisha kukonda kwa ngozi.[3] Ajenti nyingi huwa ni pamoja na mchanganyiko wa viambato hai.[9] Hivi vinaweza kuwa ni pamoja na: krimu kizuizi kama grisi au zinki oksidi, ajenti ya analijesikia kama vile lidokeni, na vasokonstrikta kama vileepinefirini.[9] Flavonoidi faida zake haziaminiki na zinaweza kudhuru.[16][9] Dalili kwa kawaida huisha kufuatia ujauzito; Kwa hivyo matibabu hucheleweshwa hadi baada ya kuzaa.[17]
Utaratibu
haririBaadhi ya taratibu zinaweza kutekelezwa ofisini. Ingawaje kwa kawaida huwa salama, madhara hatari kama vile sepsis ya kuzunguka mkundu yanaweza kutokea kwa nadra. [11]
- Ukanda wa mpira wa kufunga unapendekezwa kama mstari wa kwanza wa matibabu kwa wale walio na kiwango cha I hadi cha 3 cha ugonjwa.[11] Ni utaratibu ambapo mipira ya kunyumbulika huwekelewa kwa hemoroidi ya ndani angalau sentimita 1 juu ya mstari wa denteti ili kukatisha usafirishaji wa damu. Kati ya siku 5-7, hemoroidi zilizonyauka hupunguka. Ikiwa mpira umewekwa karibu sana na mstari wa denteti, maumivu makali hutokea punde tu baadaye.[3] Kiwango cha kutibu kimepatikana kuwa takribani 87%[3] na kiwango cha athari hadi 3%.[11]
- sklerotherapia huhusisha udungaji wa anjenti ya sklerosisi, kama vile fenoli, katika hemoroidi. Hii husababisha kuporomoka kwa kuta za vena na kunyauka kwa hemoroidi. Kiwango cha ufanisi miaka minne baada ya matibabu ni ~70 %< ref name=Review09/> Ambacho kiko juu zaidi ya kile cha kutumia ukanda wa mpira wa kufunga.[11]
- Baadhi ya njia za uunguzaji zimeonyeshanwa kuwa zinafaa kwa hemoroidi, lakini kwa kawaida hutumika tu wakati ambapo njia zingine zimefeli. Utaratibu huu unaweza kufanywa kwa kutumiaelektrokotari, mionzi ya miale isiyoonekana, upasuaji wa leza ,[3] or Upasuaji baridi.[18] Uunguzaji kwa jua inaweza kuwa suluhisho kwa ugonjwa wa kiwango cha1 au cha 2.[11] Kwa wale walio na ugonjwa wa viwango vya 3 au 4 kuna uwezekano mkubwa wa kutokea tena.[11]
Upasuaji
haririBaadhi ya mbinu za upasuaji zinaweza kutumiwa ikiwa udhibiti wa utunzaji na taratibu rahisi zitafeli.[11] Matibabu yote ya upasuji huhusishwa na kiwango fulani cha athari zikiwa ni pamoja na kuvuja damu, maambukizi, msongo wa mkundu na kubakia kwa mkojo, kwa sababu ya kukaribiana kwa rektamu kwa neva zinazosafirishia kwa utumbo.[3] Kunaweza pia kuwa na hatari ndogo ya kutoweza kuzuia kinyesi, hasa kile cha kiowevu,[19][9] with rates reported between 0% and 28%.[20][9] with rates reported between 0% and 28%.[21] * Haemoroidektomi ya ukataji ni ukataji na uondoaji wa hemoroidi unaotumika tu kwa hali hatari.[3] Unahusishwa na maumivu baada ya upasuaji yanayohisika na kwa kawaida huhitaji muda wa wiki 2–4 kupona.[3] Hata hivyo, kunazo faida za muda mrefu kwa wale walio na kiwango cha tatu cha hemoroidi ikilinganishwa na ukanda wa mpira wa kufunga.[22] Ni matibabu yaliyopendekezwa kwa wale walio na hemoroidi za nje zilizotiwa thrombasi ikiwa itafanyika kati ya muda wa masaa 24-72 .[11][6] gliserali trineteti utaratibu wa lihamu ya baadaye, husaidia kwa maumivu na uponyaji.[23]
- Yakiongozwa na-Dopla, Hemoroidi ya mkundu na ile isiyo ya uaterishaji ni matibabu madogo ya mwanzo kwa kutumia dopla ya suti iliyozidi kutambua kwa usahihi utiririkaji wa damu kwa ateri. Kisha ateri hizi ‘’hufungwa’’ na tishu iliyoshuka hurudishwa katika mahali pake pa kawaida. Ina kiwango cha juu kidogo cha kujirudia lakini inazo athari chache zikilinganishwa na hemoroidektomi. [3]
- Upasuaji wa kutoa hemoroidi iliyofunganishwa, pia inaitwa Upasuaji wa kutoa dalili za hemoroidi iliyofunganishwa, ni utaratibu unaohusisha utolewaji wa tishu nyingi za hemoroidi zilizokuwa kubwa kwa njia isiyo ya kawaida, ukifuatwa na urudishaji wa tishu za hemoroidi zilizosalia kwenye sehemu yake ya anatomi ya kawaida. Kwa kawaida huwa na maumivu madogo na huhusishwa na kupona kwa haraka ikilinganishwa na utolewaji wa kikamilifu wa hemoroidi.[3] Hata hivyo, nafasi ya hemoroidi za kidalili kurudi ni kubwa kuliko upasuaji wa kawaida wa kutoa hemoroidi[24] na kwa hivyo inapendekezwa tu kwa kiwango cha 2 au 3 cha ugonjwa.[11]
Uenezi
haririNi vigumu kutambua kiwango cha watu wanaopata hemoroidi kwa kuwa watu wengi walio nayo huwa hawaendi kumwona mhudumu wa afya.[8][5] Hata hivyo, inaaminiwa kuwa hemoroidi za kidalili huathiri angalau asilimia 50% ya idadi ya watu katika nchi ya Marekani katika wakati fulani katika maisha yao na takribani asilimia ~5% ya idadi ya watu imeathirika kwa wakati wowote unaopeanwa.[3] Jinsia zote hupitia karibu tukio sawa la hali hii[3] Huku viwango vikieleza kati ya miaka 45 na 65 .[4] Zinapatikana sana katika Kihindi[25].[9] Matokeo ya muda mrefu kwa kawaida huwa mazuri, hata kama watu wengine wanaweza kuwa na matukio ya muda mrefu yanayojirudia.[5] Kiwango kidogo tu cha watu mwishowe huhitaji upasuaji.[9]
Historia
haririUtamkwaji wa kwanza unaojulikana wa mateso haya ni kutoka 1700 KK Misri mafunjo, ambayo ushauri: “…Hupaswi kumpa mapishi, lihamu ya ukingaji mkuu; matawi ya Akeshia, chini, yakiwa yamechanganywa na kupikwa. Paka mstari wa laini hapo -kwa na uweke katika mkundu, ili apone mara moja."[26]
Katika 460 KK, Maandishi ya kusanyo wa Hipokratiki unaeleza matibabu yaliyo sawa na ukanda wa mpira wa kufunga wa kisasa: “Na hemoroidi kwa njia sawa unaweza kuzitibu kwa kuzibadili kwa sidano na kuzifunga kwa uzi sufu ulio mnene, ili upake, na usitibu mpaka zipungue na kwa kawaida uwache moja nyuma; na mgonjwa anapopona, wacha awekwe katika njia ya Hellebore.”[26]
Maelezo ya hemoroidi pia yanapatikana kwa Biblia.[27][4]
Celsus (25 KK – 14 BK) alieleza ufungaji kwa uzi na taratibu za eksisheni, na kujadili uwezekano wa athari.[28] Galen alitetea kuharibika au kwa muunganisho wa ateri kwa vena, akidai kuwa ilileta upungufu wa maumivu na kuenea kwa gangrini.[28] Susruta Samhita, (Karne ya 4 – 5AD), sawa na maneno ya Hippocrates, lakini hutilia mkazo suala la usafi wa kidonda.[26] Katika karne ya 13, madaktari wa upasuaji kutoka Ulaya kama vile Lanfranc of Milan, Guy de Chauliac, Henri de Mondeville na John wa Ardene walifanya maendeleo makuu na ukuzaji wa mbinu za upasuaji.[28]
Utumizi wa kwanza wa "hemoroidi" kwa Kiingereza ulitokea mwaka wa 1398, kutoka‘’haemoroides’’ kwa Kifaransa kutoka Kilatini hæmorrhoida -ae",[29] kwa zamu kutoka Kigiriki "αἱμορροΐς" (haimorrhois), "inayoweza kutoa damu", kutoka "αἷμα" (haima), "damu"[30] + "ῥόος" (rhoos), "mtiririko",[31] kutoka kitenzi "ῥέω" (rheo), "kutiririka".[32]
Suala la kutilia maanani
haririUkumbi-wa-mchezaji maarufu wa besiboli George Brett alitolewa mchezoni katika mfululizo wa dunia1980 kwa sababu ya maumivu ya hemoroidi. Baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo, Brettvalirudi kucheza mchezo uliofuata, akisema "...shida zangu zote ziko nyuma yangu."[33] Brett underwent further hemorrhoid surgery the following spring.[34] mtoaji maoni ya kisiasa anyeshikilia mambo Glenn Beck alifanyiwa upasuaji wa hemoroidi, baadaye akaeleza tukio alilopitia lisilopendeza katika video YouTube inayotazamwa sana ya mwaka wa 2008s.[35]
Marejeo
hariri- ↑ Chen, Herbert (2010). Illustrative Handbook of General Surgery. Berlin: Springer. uk. 217. ISBN 1-84882-088-7.
- ↑ 2.00 2.01 2.02 2.03 2.04 2.05 2.06 2.07 2.08 2.09 2.10 2.11 2.12 2.13 2.14 Schubert, MC; Sridhar, S; Schade, RR; Wexner, SD (2009). "What every gastroenterologist needs to know about common anorectal disorders". World J Gastroenterol. 15 (26): 3201–9. doi:10.3748/wjg.15.3201. ISSN 1007-9327. PMC 2710774. PMID 19598294.
{{cite journal}}
: Unknown parameter|month=
ignored (help)CS1 maint: unflagged free DOI (link) - ↑ 3.00 3.01 3.02 3.03 3.04 3.05 3.06 3.07 3.08 3.09 3.10 3.11 3.12 3.13 3.14 3.15 3.16 3.17 3.18 3.19 3.20 3.21 3.22 3.23 Lorenzo-Rivero, S (2009). "Hemorrhoids: diagnosis and current management". Am Surg. 75 (8): 635–42. PMID 19725283.
{{cite journal}}
: Unknown parameter|month=
ignored (help) - ↑ 4.00 4.01 4.02 4.03 4.04 4.05 4.06 4.07 4.08 4.09 4.10 4.11 4.12 4.13 4.14 4.15 4.16 4.17 4.18 Kaidar-Person, O (2007 Jan). "Hemorrhoidal disease: A comprehensive review" (PDF). Journal of the American College of Surgeons. 204 (1): 102–17. PMID 17189119. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2012-09-22. Iliwekwa mnamo 2013-11-28.
{{cite journal}}
: Check date values in:|date=
(help); Unknown parameter|=
ignored (help); Unknown parameter|coauthors=
ignored (|author=
suggested) (help); Unknown parameter|dead-url=
ignored (|url-status=
suggested) (help) - ↑ 5.0 5.1 5.2 5.3 5.4 Davies, RJ (2006 Jun). "Haemorrhoids". Clinical evidence (15): 711–24. PMID 16973032.
{{cite journal}}
: Check date values in:|date=
(help) - ↑ 6.0 6.1 6.2 6.3 6.4 Dayton, senior editor, Peter F. Lawrence; editors, Richard Bell, Merril T. (2006). Essentials of general surgery (tol. la 4th ed.). Philadelphia ;Baltimore: Williams & Wilkins. uk. 329. ISBN 9780781750035.
{{cite book}}
:|edition=
has extra text (help);|first=
has generic name (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link) - ↑ Azimuddin, edited by Indru Khubchandani, Nina Paonessa, Khawaja (2009). Surgical treatment of hemorrhoids (tol. la 2nd ed.). New York: Springer. uk. 21. ISBN 978-1-84800-313-2.
{{cite book}}
:|edition=
has extra text (help);|first=
has generic name (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link) - ↑ 8.0 8.1 Reese, GE (2009 Jan 29). "Haemorrhoids". Clinical evidence. 2009. PMID 19445775.
{{cite journal}}
: Check date values in:|date=
(help); Unknown parameter|coauthors=
ignored (|author=
suggested) (help) - ↑ 9.00 9.01 9.02 9.03 9.04 9.05 9.06 9.07 9.08 9.09 Beck, David (2011). The ASCRS textbook of colon and rectal surgery (tol. la 2nd ed.). New York: Springer. ku. 174–177. ISBN 9781441915818.
{{cite book}}
:|edition=
has extra text (help) Hitilafu ya kutaja: Invalid<ref>
tag; name "ASCRS2011" defined multiple times with different content - ↑ National Digestive Diseases Information Clearinghouse (2004). "Hemorrhoids". Chuo cha kitaifa cha maradhi ya sukari na yale ya ummeng’enyo na figo (NIDDK), NIH. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-03-23. Iliwekwa mnamo 18 Machi 2010.
{{cite web}}
: Unknown parameter|month=
ignored (help) - ↑ 11.00 11.01 11.02 11.03 11.04 11.05 11.06 11.07 11.08 11.09 11.10 11.11 Rivadeneira, DE (2011 Sep). "Practice parameters for the management of hemorrhoids (revised 2010)". Diseases of the colon and rectum. 54 (9): 1059–64. PMID 21825884.
{{cite journal}}
: Check date values in:|date=
(help); Unknown parameter|coauthors=
ignored (|author=
suggested) (help) - ↑ Frank J Domino (2012). The 5-Minute Clinical Consult 2013 (Griffith's 5 Minute Clinical Consult). Hagerstown, MD: Lippincott Williams & Wilkins. uk. 572. ISBN 1-4511-3735-4.
- ↑ Glass, [edited by] Jill C. Cash, Cheryl A. Family practice guidelines (tol. la 2nd ed.). New York: Springer. uk. 665. ISBN 9780826118127.
{{cite book}}
:|edition=
has extra text (help);|first=
has generic name (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link) - ↑ 14.0 14.1 Alonso-Coello, P.; Guyatt, G. H.; Heels-Ansdell, D.; Johanson, J. F.; Lopez-Yarto, M.; Mills, E.; Zhuo, Q.; Alonso-Coello, Pablo (2005). Alonso-Coello, Pablo (mhr.). "Laxatives for the treatment of hemorrhoids". Cochrane Database Syst Rev (4): CD004649. doi:10.1002/14651858.CD004649.pub2. PMID 16235372.
- ↑ {{cite journal|last=Lang|first=DS|coauthors=Tho, PC; Ang, EN|title=Effectiveness of the Sitz bath in managing adult patients with anorectal disorders|journal=Japan journal of nursing science : JJNS|date=2011 Dec|volume=8|issue=2|pages=115-28|pmid=22117576}}
- ↑ Alonso-Coello P, Zhou Q, Martinez-Zapata MJ; na wenz. (2006). "Meta-analysis of flavonoids for the treatment of haemorrhoids". Br J Surg. 93 (8): 909–20. doi:10.1002/bjs.5378. PMID 16736537.
{{cite journal}}
: Explicit use of et al. in:|author=
(help); Unknown parameter|month=
ignored (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link) - ↑ Quijano, CE (2005 Jul 20). "Conservative management of symptomatic and/or complicated haemorrhoids in pregnancy and the puerperium". Cochrane database of systematic reviews (Online) (3): CD004077. PMID 16034920.
{{cite journal}}
: Check date values in:|date=
(help); Unknown parameter|coauthors=
ignored (|author=
suggested) (help) - ↑ Misra, MC (2005). "Drug treatmentof haemorrhoids". Drugs. 65 (11): 1481–91. PMID 16134260.
{{cite journal}}
: Unknown parameter|coauthors=
ignored (|author=
suggested) (help)CS1 maint: extra punctuation (link) - ↑ Pescatori, M (2008 Mar). "Postoperative complications after procedure for prolapsed hemorrhoids (PPH) and stapled transanal rectal resection (STARR) procedures". Techniques in coloproctology. 12 (1): 7–19. PMID 18512007.
{{cite journal}}
: Check date values in:|date=
(help); Unknown parameter|coauthors=
ignored (|author=
suggested) (help) - ↑ {{citename="Pescatori 2008">Pescatori, M (2008 Mar). "Postoperative complications after procedure for prolapsed hemorrhoids (PPH) and stapled transanal rectal resection (STARR) procedures". Techniques in coloproctology. 12 (1): 7–19. PMID 18512007.
{{cite journal}}
: Check date values in:|date=
(help); Unknown parameter|coauthors=
ignored (|author=
suggested) (help) - ↑ Ommer, A (2008 Nov). "Continence disorders after anal surgery--a relevant problem?". International journal of colorectal disease. 23 (11): 1023–31. PMID 18629515.
{{cite journal}}
: Check date values in:|date=
(help); Unknown parameter|coauthors=
ignored (|author=
suggested) (help) - ↑ Shanmugam, V (2005 Jul 20). "Rubber band ligation versus excisional haemorrhoidectomy for haemorrhoids". Cochrane database of systematic reviews (Online) (3): CD005034. PMID 16034963.
{{cite journal}}
: Check date values in:|date=
(help); Unknown parameter|coauthors=
ignored (|author=
suggested) (help) - ↑ Ratnasingham, K (2010). "Meta-analysis of the use of glyceryl trinitrate ointment after haemorrhoidectomy as an analgesic and in promoting wound healing". International journal of surgery (London, England). 8 (8): 606–11. PMID 20691294.
{{cite journal}}
: Unknown parameter|coauthors=
ignored (|author=
suggested) (help) - ↑ Jayaraman, S (2006 Oct 18). "Stapled versus conventional surgery for hemorrhoids". Cochrane database of systematic reviews (Online) (4): CD005393. PMID 17054255.
{{cite journal}}
: Check date values in:|date=
(help); Unknown parameter|coauthors=
ignored (|author=
suggested) (help) - ↑ Christian Lynge, Dana; Weiss, Barry D. (2001). 20 Common Problems: Surgical Problems And Procedures In Primary Care. McGraw-Hill Professional. uk. 114. ISBN 978-0-07-136002-9.
- ↑ 26.0 26.1 26.2 Ellesmore, Windsor (2002). "Surgical History of Haemorrhoids". Katika Charles MV (mhr.). Surgical Treatment of Haemorrhoids. London: Springer.
- ↑ King James Bible. 1 Samuel 6 4.
{{cite book}}
: CS1 maint: location (link) - ↑ 28.0 28.1 28.2 Agbo, SP (1 Januari 2011). "Surgical management of hemorrhoids". Journal of Surgical Technique and Case Report. 3 (2): 68. doi:10.4103/2006-8808.92797.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: unflagged free DOI (link) - ↑ hæmorrhoida, Charlton T. Lewis, Charles Short, A Latin Dictionary, on Perseus Digital Library
- ↑ αἷμα, Henry George Liddell, Robert Scott, A Greek-English Lexicon, on Perseus Digital Library
- ↑ ῥόος, Henry George Liddell, Robert Scott, A Greek-English Lexicon, on Perseus Digital Library
- ↑ ῥέω, Henry George Liddell, Robert Scott, A Greek-English Lexicon, on Perseus Digital Library
- ↑ Dick Kaegel. "Memories fill Kauffman Stadium", Major League Baseball, March 5, 2009. Retrieved on 2013-11-28. Archived from the original on 2011-06-05.
- ↑ "Brett in Hospital for Surgery", The New York Times, March 1, 1981.
- ↑ "Glenn Beck: Put the 'Care' Back in Health Care", Jan. 8, 2008. Retrieved on 17 September 2012.
Viungo vya nje
hariri- Bawasiri katika Open Directory Project