Henry III wa Uingereza
Henry III (1 Oktoba 1207 – 16 Novemba 1272) alikuwa mfalme wa Uingereza mwaka 1216 alipokuwa na umri wa miaka 9. Alitawala kama mfalme wa Uingereza na mkuu wa Eire hadi kifo chake kwenye mwaka 1272. Alimwoa Eleanor wa Provence. Alianzisha majengo katika mtaa wa Westminster mjini London ulioendelea kuwa makao ya serikali ya Uingereza kwa karne nyingi.
Miaka mingi aligombana na makabaila wakubwa juu ya haki za mfalme. Alipaswa kuthibitisha sheria ya Magna Charta na kukubali makao ya bunge ya kwanza ya Uingereza mwaka 1264 iliyokuwa na haki ya kukubali au kukataa kodi.
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Henry III wa Uingereza kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |