Hifadhi ya Mazingira ya Abuko

eneo la ulinzi

Hifadhi ya Kitaifa ya Abuko ni hifadhi ya asili nchini Gambia iliyo kusini mwa mji wa Abuko . Ni kivutio maarufu cha watalii na ilikuwa hifadhi ya kwanza ya wanyamapori kuteuliwa nchini.

Kibao kinacho onyesha Hifadhi ya Kitaifa ya Abuko

Historia hariri

Eneo hilo lilipewa ulinzi kwa mara ya kwanza mwaka 1916 wakati Mkondo wa Lamin, unaopita kwenye hifadhi hiyo, ulipowekewa uzio ili kuunda kituo cha kukusanya maji. [1] Uzio wa mkondo huo ulipelekea ongezeko la akiba ya wanyamapori na mimea msituni.

Mnamo 1967 afisa wa wanyamapori Eddie Brewer na bintiye Stella Marsden walitembelea eneo hilo na kutambua umuhimu wa uhifadhi wa msitu na wanyamapori wake. Brewer alitoa ombi kwa serikali ili eneo hilo lilindwe. [2] Mnamo 1968 Idara ya Wanyamapori, sasa Idara ya Hifadhi na Usimamizi wa Wanyamapori ya Gambia ilianzishwa kwenye hifadhi. [3]

Picha hariri

Marejeo hariri