Historia ya Azerbaijan

Historia ya Azerbaijan inahusu eneo ambalo leo linaunda jamhuri ya Azerbaijan.

Michoro ya miambani ya milenia ya 10 KK katika Gobustan National Park, ambayo imeorodheshwa na UNESCO kuwa Urithi wa Dunia.

Azerbaijan ina historia ndefu kuanzia Zama za Mawe.

Kuanzia karne ya 9 KK ilikaliwa na Washitia, halafu Wamedi, wote wa jamii ya Waajemi ambao walishinda na kuunda dola kubwa kati ya karne ya 6 KK. Tangu hapo Uzoroastro ulienea nchini.

Baadaye eneo hilo liliingizwa katika Ugiriki wa Kale chini ya Aleksanda Mkuu hadi karne ya 4 KK wakazi wa Kaukazi walianzisha ufalme wa kwao ambao katika karne ya 4 BK ulipokea Ukristo kama dini rasmi.

Kwa kuwa ufalme huo kuanzia mwaka 252 ulikuwa chini ya himaya ya Dola la Wasasanidi wa Uajemi, hao waliposhindwa na Waarabu Waislamu, Azerbaijan iliingia bila kutaka katika mtandao wao (667).

Kuanzia mwaka 1067 watu wa jamii ya Waturuki walianza kuenea nchini pamoja na lugha yao.

Mwanzoni mwa karne ya 19 Urusi iliteka eneo hilo kutoka kwa Waajemi.

Jaribio la Kaukazi Kusini kujitenga baada ya vita vikuu vya kwanza lilishindikana mwaka 1918. Vilevile jaribio kama hilo la Azerbaijan peke yake lilikomeshwa mwaka 1920.

Hatimaye uhuru ulipatikana mwaka 1991, kwa Umoja wa Kisovyeti kusambaratika.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Azerbaijan kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.