Historia ya Indonesia

Historia ya Indonesia inahusu eneo ambalo leo linaunda Jamhuri ya Indonesia.

Visiwa vya Indonesia viliathiriwa na utamaduni wa Uhindi. Kisiasa kulikuwa na falme nyingi.

Tangu karne ya 17 Waholanzi walianza kujenga vituo na kueneza utawala wao. Waliita koloni lao "Uhindi wa Kiholanzi" ("Nederlands-Indië").

Wakati wa vita vikuu vya pili vya dunia Japani ikatwaa visiwa na kuwafukuza Waholanzi.

Mwisho wa vita kiongozi Sukarno akatangaza Indonesia kama nchi huru. Waholanzi walijaribu kurudisha utawala wao lakini walilazimishwa na Marekani kukubali uhuru wa nchi.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Indonesia kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.