Hivi Ama Vile
"Hivi-Ama-Vile" (pia unajulikana kama Watani wa Jadi) ni jina la wimbo uliotoka 18 Agosti, 2017 wa wasanii wa muziki wa hip hop kutoka nchini Tanzania - Rostam, yaani Roma na Stamina ndiyo kifupi cha Rostam. Wimbo umetayarishwa na Mr. T. Touch ukiwa wimbo wa kwanza kutolewa kama Rostam. Wimbo una majibizano ya nani ni nani, na nani zaidi kuliko nani. Wametajwa wasanii, wanasiasa na watu wengine wenye athira kubwa katika jamii ya Watanzania. Wimbo umetoka siku nane tangu kutolewa wimbo wa Roma wa "Zimbabwe", yaani ulitoka tarehe 10 Agosti 2017 na huu ukatoka tarehe 18 Agosti 2017. Video ya wimbo huu umeongozwa na Nicklass aliyeongoza wimbo wa Zimbabwe pia.
“Hivi Ama Vile” | |||||
---|---|---|---|---|---|
Kava la Hivi Ama Vile
| |||||
Single ya Roma na Stamina Rostam | |||||
Imetolewa | 18 Agosti, 2017 | ||||
Muundo | Upakuzi mtandaoni | ||||
Imerekodiwa | 2017 | ||||
Aina | Hip hop | ||||
Urefu | 3:28 | ||||
Studio | Babaz Entertainment | ||||
Mtunzi | Roma Stamina | ||||
Mtayarishaji | Mr. T. Touch | ||||
Mwenendo wa single za Roma na Stamina Rostam | |||||
|
Tazama pia
haririMarejeo
haririViungo vya nje
hariri- Hivi Ama Vile katika YouTube