Homa ya Lassa (kwa Kiingereza: Lassa hemorrhagic fever), ni aina ya homa inayosababishwa na virusi vya Lassa.

Dalili za homa hii huanza kuonekana baada ya muda wa wiki mbili na kuendelea. Wakati dalili zinapoanza kuonekana mambo yafuatayo yanatokea: homa, udhaifu, maumivu ya kichwa, kutapika, na maumivu ya misuli, kutokwa na damu mdomoni.

Hatari zaidi ni kifo mara moja ambapo umeambukizwa na hujapata matibabu ndani ya wiki tatu.

Robo ya wale wanaoishi baada ya ugonjwa kwisha huwa wamepoteza uwezo wa kusikia.

Mara nyingi ugonjwa huenea kwa watu kwa njia ya mgusano na mkojo au kinyesi cha panya au kushika panya aliyekufa. Kuenea kunaweza kutokea pia kupitia mawasiliano ya moja kwa moja baina ya watu.

Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Homa ya Lassa kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.