Huduma za Maktaba Tanzania

Huduma za Maktaba Tanzania zinahusu watu kufaidika na Maktaba, mikusanyo wa vitabu na visikiziona, vilivyowekwa kwa utaratibu maalum kwa ajili ya kusoma, kujifunza na ushauri.

Hivyo maktaba ni kiunganishi kikubwa kati ya wasomaji ama watumiaji wa machapisho.Aidha maktaba ni chombo cha mawasiliano kwa kuwa kazi zake ni pamoja na kukusanya habari, kutengeneza na kutunza kwa manufaa ya kizazi kijacho na kutawanya habari hizo kwa wahitaji.

Nchini Tanzania kuna aina mbalimbali za huduma za maktaba. Huduma hizi ni pamoja na huduma za maktaba za taifa, maktaba za umma, za vyuo vikuu, za vyuo vingine na za shule (yaani shule za msingi and sekondari). Kwenye ngazi ya kitaifa, serikali ya Tanzania limeanzisha Shirika la Huduma za Maktaba.

Maktaba ya Taifa

hariri

Maktaba za Vyuo Vikuu

hariri

Maktaba za Shule

hariri

Maktaba za skuli/shule huwa na vifaa mbalimbali vinavyotoa taarifa, kuelimisha na kuburudisha. Maktaba hizi hutoa huduma kwa walimu na wanafunzi. Maktaba za skuli ni viungo muhimu katika kukamilisha malengo ya elimu ya msingi na sekondari nayo ni kumtayarisha mwanafunzi kuwa raia bora katika jamii yake na taifa kwa ujumla. Kumwezesha na kumkuza mtumiaji wake kuwa na tabia ya kuendelea kujifunza mwenyewe, kuwa na uwezo wa kutafiti, kudadisi, kubuni na kuhoji pamoja na kufanya uchambuzi na kutathmini hali ya mambo na kufanya maamuzi sahihi. Kubwa zaidi ni kuwa na uwezo wa kukabiliana na matatizo mbalimbali yatayomkabili katika maisha yake ya kila siku.Maktaba za skuli zinatarajiwa kuwa na mkusanyiko wa vitabu vya ziada na kiada kwa masomo yote, vitabu vya rejea, mihtasari ya masomo, atlasi, machati, vitabu vya hadithi mbalimbali, kazi zilizofanywa na wanafunzi, karatasi za mitihani iliyopita, ramani mbalimbali za nchi na dunia, nakadhalika.

Jambo la kutiliwa mkazo wa kipekee ni kuweka vifaa vya kisasa vya kufundishia na kutolea taarifa katika maktaba hizo. Vifaa kama vile komputa, televisheni, projekta, redio, kanda za redio na video, CD na DVD vitasaidia sana kuamsha hamu ya wanafunzi kutembelea maktaba mara kwa mara.

Hali ya maktaba za skuli nchini

hariri

Kwa mujibu wa Shirika la Huduma za Maktaba Zanzibar, takriban asilimia sitini (60%) ya skuli za msingi hazina maktaba wakati asilimia sabini (70%) ya skuli za sekondari zinaonekana kuwa na maktaba. Takwimu hizi zinaonesha kuwa suala la maktaba bado halijapewa umuhimu wake unaostahili katika skuli za msingi, skuli ambazo kama jina lake zinatarajiwa kumjengea msingi madhubuti mwanafunzi aliyepata elimu ya msingi ili aweze kuhimili vishindo vya elimu ya sekondari kama atapata fursa ya kuendelea au kumtayarisha kuwa raia mwema katika jamii yake aweze kuishi kwa matumaini na kujitegemea ikiwa atamalizia elimu ya msingi.

Kwa upande mwengine skuli za sekondari kwa kiasi kikubwa huwa na maktaba. Suali la kujiuliza je, maktaba hizi zinakidhi haja za watumiaji wake?

Kwa ufupi, maktaba nyingi za skuli za sekondari hazikidhi haja za watumiaji wake hali hii inajitokeza katika upande wa mazingira, vifaa, wafanyakazi na matumizi/huduma zinazotolewa katika maktaba hizo.[1][2]

Marejeo

hariri
  1. Omar, Abbas M. (2010). The Teacher's role in Fostering Independent Learning in High Schools in Zanzibar.
  2. Omar, Abbas Mohamed (2013-12-01). "The teachers' role in fostering independent learning in high schools in Zanzibar". IFLA Journal (kwa Kiingereza). 39 (4): 311–318. doi:10.1177/0340035213509223. ISSN 0340-0352.
  Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Huduma za Maktaba Tanzania kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.