I Stay in Love
"I Stay in Love" ni wimbo uliandikwa na Mariah Carey, Bryan-Michael Cox, WyldCard, wakishirikiana na Roderick Hollingsworth kwa ajili ya albamu ya studio kutoka kwa Carey ya kumi na moja E=MC². Albamu hii iliandaliwa na Carey akishirikiana na Cox. Wimbo wa Stay in Love ulitolewa kama single ya nne na ya mwisho kutoka katika albamu hii. Wimbo huu ulichezwa katika tuzo za American Music Award zilizofanyika tarehe 23 Novemba 2008. Wimbo huu ilifanikiwa kufika nafasi ya kwanza katika chati ya Billboard Hot Dance Club Play.[1]
“I Stay In Love” | |||||
---|---|---|---|---|---|
Single ya Mariah Carey | |||||
Muundo | Digital download, CD single | ||||
Aina | Pop, R&B | ||||
Urefu | 3:32 | ||||
Studio | Island Def Jam | ||||
Mtunzi | Mariah Carey, Bryan-Michael Cox, WyldCard, Roderick Hollingsworth | ||||
Mtayarishaji | Bryan-Michael Cox, Mariah Carey | ||||
Mwenendo wa single za Mariah Carey | |||||
|
Mapokezi
haririWadadisi wa mambo wanasema kuwa wimbo wa I Stay in Love ulipata mapokezi mazuri, katika kupitia matokeo ya albamu hii ya E=MC², Toleo la katika wavuti juu ya wimbo huu The Republican yanasema kuwa Carey anang'ara katika wimno huu,[2] wakati Fox News Channel akiuelezea wimbo huu kama wenye mashairi mazito,
Matangazo
haririCarey aliimba wimbo katika onesho la moja kwa moja lililofanyika nchini Uingereza la vipaji linalojulikana kama The X Factor tarehe 8 Novemba 2008, ikiwa ni pamoja na kuimba wimbo wa "Hero" na washiriki wa enesho hilo. Pia aliumba wimbo huu katika onesho la tuzo za American Music Award lililofanyika tarehe 23 Novemba 2008 katika eneo la Nokia Theatre.[3][4]
Video ya Muziki
haririIkiongozwa na mumewe Carey aitwaye Nick Cannon, video ya muziki hii ilitengenezwa katika eneola Las Vegas, Nevada, kwa kutumia hadithi ambayo Cannon na Carey waliwahi kushiriki kuiandika [5] Carey alipiga picha kwa ajili ya video hii katika ukumbi usiku katika hoteli ya Bellagio tarehe 5 Oktoba 2008.[6][7][8] Carey aliendelea na upigaji picha kwa ajili ya video ya wimbo huu tarehe 6 Oktoba 2008, katika jangwa la Mojave. Akiwa katika mohajiano na Ryan Seacrest, Cannon akiongea kuhusu video hii anasema kuwa, kuna wakati ambapo Carey anakuwa katika kitanda na mwanaume( aliyecheza nafasi hiyo alikuwa Andrew Karelis),...."[9]
Video hii iliingia katika chati ya Billboard na kushika nafasi ya 16 tarehe 6 Desemba 2008.
Orodha ya nyimbo na muundo
hariri- U.S. Digital Remix
- "I Stay In Love" (Jody den Broeder Radio Edit) – 4:08
- "I Stay In Love" (Ralphi Rosario Melodic Radio Edit) – 3:50
- "I Stay In Love" (Jody den Broeder House Mix) – 8:29
- "I Stay In Love" (Ralphi Rosario Big Vocal) – 8:12
Chati
haririWimbo huu uliingia katika chati ya Billboard Hot R&B/Hip-Hop Songs na kufikia katika nafasi ya 97 hii ikiwa ni tarehe 15 Novemba 2008 na kupanda hadi kufikia nafasi ya 81.[10] Single hii iliingia katika chati ya Billboard ya Rhythmic Airplay Chart katika nafasi ya 38 tarehe 20 Desemba na kuoanda hadi nafasi ya 37 tarehe 27 mwezi huo huo, 2008. Pia wimbo huu ulishika nafasi ya 4 katika chati ya Billboard ya Marekani ya Hot 100 Singles Sales. Na kufikia mwishoni mwa mwezi Desemba, wimbo huu ulikuwa katika nafasi ya 81.
Chati
haririChati (2008) | Ilipata nafasi |
---|---|
UK Singles (The Official Charts Company)[11] | 95 |
US Hot Dance Club Songs (Billboard)[12] | 1 |
US Hot R&B/Hip-Hop Songs (Billboard)[13] | 81 |
Historia ya kutoka
haririEneo | Tarehe | Muundo |
---|---|---|
Marekani | 28 Oktoba 2008 | Airplay |
Marekani, Kanada | 16 Desemba 2008 | Digital download |
Marejeo
hariri- ↑ "Billboard". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-03-17. Iliwekwa mnamo 2006-03-17.
- ↑ O'Hare, Kevin. Carey gets the Formula Right on 'E=MC2'. MassLive.com. 13 Aprili 2008. Retrieved 6 Oktoba 2008.
- ↑ Mariah Carey to Perform at the American Music Awards Ilihifadhiwa 20 Aprili 2010 kwenye Wayback Machine.. People. 10 Novemba 2008. Retrieved 12 Novemba 2008.
- ↑ Mariah to Perform at 36th Annual "American Music Awards" November 23 on ABC Ilihifadhiwa 12 Novemba 2008 kwenye Wayback Machine.. MariahCarey.com. 11 Novemba 2008. Retrieved 12 Novemba 2008.
- ↑ Mariah Set to Shoot Video for New Single I Stay In Love Ilihifadhiwa 8 Desemba 2008 kwenye Wayback Machine.. MariahCarey.com. Tuesday, 3 Oktoba 2008. Retrieved Tuesday, 3 Oktoba 2008.
- ↑ Clarke, Norm. NORM: Bobbitt trains for boxing bout in LV. Las Vegas Review-Journal. 6 Oktoba 2008. Retrieved 6 Oktoba 2008.
- ↑ [1]
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-12-11. Iliwekwa mnamo 2010-01-26.
- ↑ [2]
- ↑ "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2006-03-17. Iliwekwa mnamo 2006-03-17.
- ↑ "Chart Stats – Mariah Carey – {{{song}}}" UK Singles Chart. Chart Stats.
- ↑ "Mariah Carey Album & Song Chart History" Billboard Hot Dance/Club Play for Mariah Carey. Prometheus Global Media.
- ↑ "Mariah Carey Album & Song Chart History" Billboard R&B/Hip-Hop Songs for Mariah Carey. Prometheus Global Media.